Naenda Kuwaandalia Mahali - I Go Prepare a Place for you

Maandiko yote yaliyotumika ni NKJV isipokuwa kama yamebainishwa vinginevyo

 Muhtasari: Yeshua alisema, “ Naenda kuwaandalia mahali”. Huu ujumbe unaeleza mshikamano wa ajabu wa Yohana 14 na Pentekoste. Je, twaenda mbinguni kuolewa au la? Pentekoste inahusianaje na arusi ya Mungu aliye hai! Jifunze jinsi arusi ya siku za Yesu inaonyesha analofanya Mungu ili Mwanawe awe na nyumba nzuri ya Bi Arusi wakati atakapomuoa. Karamu ya Arusi hii itafanyika wapi? Nyumba hii ya kifahari na kao la Bi arusi liko wapi? Je, wanawali wale kumi wa Mathayo 25 wanafanana na Bi arusi? Na haya yote yana uhusiano gani na Pentekoste? Ni wakati wa kujua!

[KUMBUKA: Maelezo haya ni sawa na yale yaliyosemwa kwa sauti. Ninapendekeza sana usikilize sauti hata unapofuatilia pamoja na maelezo haya. Kutakuwa na mambo yaliyosemwa kwenye sauti yasiyo kwenye maelezo - - na labda kinyume chake. Ilinibidi nizungumze haraka na kusonga kwa upesi sana, kwa hivyo itakuwa na manufaa kuwa na maandiko yaliyochapishwa katika nakala hii. Furahia ujumbe!! [Philip Shields]

Siku njema, ndugu na dada wa Nyumba ya Baba, washiriki wa mwili wa Yesu Kristo – au kama vile ninavyomuita, Yeshua. Na salamu za furaha kwa yeyote aliye na sehemu kwa Bibi arusi wa mwana wa Mungu.

Leo, sikukuu ya Pentekoste ni karibu sana. Ni siku takatifu ya kufurahisha na pia sikukuu ya Mungu. Nitajadili mambo kadhaa ya kawaida ambayo hayajaguzwa kuhusu Pentekoste. Ikiwa unataka maelezo kamili ya mavuno madogo ya msimu wa joto na maana yake, basi tafadhali angalia mahubiri yangu juu ya Pentekoste tokea miaka iliyopita.

Siku hii Mungu wa Milele alizungumza Torati yake, sheria, kwa tarumbeta kubwa ya Mungu na kwa sauti yake mwenyewe. Ilikuwa pia siku hii wakati Mungu yuyo huyo alimtuma Roho wake kwa wale waliokusanyika wapatao 120 huko Yerusalemu.

Ninaamini pia Yohana 14:1-3 ina uhusiano mwingi kwa siku hii ya Pentekoste. Yohana 14: 1-4. Ni hadithi kubwa zaidi ya upendo iliyowahi kunenwa. Kile nitakachokishughulikia sio cha kipekee kwangu, lakini kimejadiliwa na kuchunguzwa na wanafunzi wengi wa Biblia, lakini linafaa kukaguliwa. Zaidi ya hayo kawaida tunajifunza zaidi na zaidi juu ya mafungu haya kadri miaka inavyopita. Natumai leo, pia, utajifunza zaidi

Yohana 14:1-4

" Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi[au makazi; maeneo ya makazi]; kama sivyo, ningaliwaambia. Naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia..”

 Hii inaelezewa kama mahali petu. Mahali “penu. ” Wakati Mungu atatayarisha mahali, patafanywa pema na pazuri. Nimekuwa kwenye safari za Tuzo zilizotayarishwa kwa uangalifu ulimwenguni kote, hata kwenye chakula cha jioni maalum kilichopeanwa kwenye jumba la Prague, lakini hizo hazitakuwa chochote kikilinganishwa na kile Baba na Mwana wake wanatuandalia.

Ninashughulikia hili kwa sababu naamini lina yote yanayohusiana na Pentekoste. Kile Mungu anatuandalia kinapita zaidi ya matarajio yetu ya ndani. Ndio, kuna maana ya mavuno madogo ya machipuko yanayoonyesha wale wanaoitwa kwanza. Halafu kuna mavuno makubwa ya Mapukutiko kwa matunda, mboga na zabibu zinazoonyesha mavuno ya wanadamu wengine katika Milenia na zaidi. Nitakuuliza uangalie tovuti yangu katika miaka iliyopita ili usikie ujumbe huo.

Ingawa HIYO maana ya Pentekoste –pia inaitwa Sikukuu ya Malimbuko ya Kwanza, Sikukuu ya Majuma ( Sabato ) – ni mada halali KABISA ya siku, tusisahau maana zingine. Kwa kuwa maana ya mavuno madogo ya kwanza yamenenwa sana, nitatumia wakati wangu kwa zilizojadiliwa kidogo leo – japo ni MAANA AMBAYO INAPASWA kuturudisha kwa kweli na kutufurahisha! Sielewi kwa nini mahubiri ya sikukuu mara nyingi yanakuwa kavu sana, yenye kurudiwa na yanachosha kusema kweli. HAIPASWI kuwa hivyo kabisa!

Natumai wakati nitakapomaliza haya utaona Yerusalemu ya juu katika nuru mpya.

Pentekoste- Wakati wa ARUSI na Ndoa katika nyakati za Biblia

Pentekoste, au ikikaribia Pentekoste, ndipo wakati ambapo pia Yahweh alioa Israeli. Ninasema “ ikikaribia Pentekoste ” kwa sababu haiwezi kudhibitishwa kabisa kuwa yote yalifanyika kwenye Pentekoste, lakini wakati huo unafaa. Mapokeo ya Kiyahudi yanasema vivyo hivyo, ingawa siendani kila wakati na yale yanayonenwa na mapokeo ya Wayahudi.

Msimu wa Pentekoste pia ulikuwa wakati ambapo Boazi na Ruthu walioana – pia inaonyesha Mungu akioa kanisa. Ni ya ajabu kutambua kwamba Ruthu alikuwa Mmoabu ambaye alikuwa amemkubali Mungu wa Israeli, hii inaonyesha wakati ambapo Israeli wa kiroho wangeundwa na washiriki wa mataifa yote, hasa pamoja na watu wa Mataifa. Natumai kuwa na wakati wa kuwa na mahubiri kamili kwenye kitabu cha Ruthu / Pentecoste. Utarajie kuyatazama hayo.

Pentekoste katika Matendo 2 pia ni wakati ambapo Mungu alituma arraboni – Kigiriki inamaanisha bidii, dhamana, malipo ya amana. Huko Ugiriki, neno la Kiyunani la kisasa la “pete ya ushiriki ” ni arrabona. Kwa hiyo siku hii Mungu alijishirikisha, au akawaposa, waumini wa Agano Jipya. Nadhani ni jambo la busara kuamini kwamba Baba pia siku hiyo atafanya arusi ya ajabu kwa Mwana wake na kukamilisha amana. Kumbuka ilikuwa wakati au ikikaribia Pentekoste ambapo Mungu alioa Israeli huko Sinai. Naamini kwamba itakuwa siku hiyo ambapo hatutaposwa tu, bali tutaolewa.

Kabla ya mahubiri haya kumalizika, natumai utaona Yerusalemu ya mbinguni kwa nuru mpya. Tazama Yeshua anasema anaenda mahali anapotuandalia kisha atatuleta huko. Je, alienda wapi?   Itakuwa mahali pa Bibi arusi. Anapaita “ mahali penu ”. Yeshua basi anasema, “ Haya, nawataka mkae huko mahali niliko. ”

Maporomoko ya Niagara na safari za tuzo

Yote tunayo hivi sasa ni baadhi ya vilele vya “ chakumbimbi ”. Hadithi juu ya jinsi baba yangu alivyotufanya tufumbe macho yetu wakati anatutembeza ufuoni mwa Maporomoko ya Niagara, ambapo maji yalikuwa yakiteleza

ukingoni. Alitaka kuona jinsi tulivyoshangaa. Mungu huturuhusu tuone mng’aro mdhaifu tu ya kile alichonacho kwetu hadi sasa. Kile anachopanga kitakuwa zaidi ya ndoto zetu za ajabu.

Kumbuka fungu kuhusu “ jicho halijaona ... vitu ambavyo Mungu ameandalia wale wanaompenda ”? Siku hii, naamini, ni zaidi ya mavuno tu. Ni siku ya kufurahia, na kufurahisha. Mahubiri ya sikukuu yanapaswa kuwa mahubiri ya kufurahisha! Kile ambacho Mungu anatuandalia kitakuwa cha kushangaza kwetu. Hautataka kukikosa.

Kwa hivyo alienda wapi kutuandalia mahali? Mara baada ya kufufuka kwake, alimwambia Maria Magdalene katika Yohana 20 kwamba alikuwa akienda kwa baba yake na baba ya Maria! Alikuwa anarudi mbinguni kama utimilifu halisi wa mganda unaotikiswa.

Yohana 14: 2 pia ananena juu ya “ makao ”. Kiyunani ni makazi, maeneo ya makazi – kama tafsiri nyinginezo zinavyoonyesha. Ni neno lile lile lililotumiwa katika Yohana 14:23- ambapo Mungu anakuja kukaa ndani yetu, kutufanya tuwe makao yake. Inahusu nyumbani, mahali unapoishi. Nyumbani kwetu, mji wetu. Haimaanishi “ ofisi ” nafasi au na cheo, kama vile wengine walivyotuongoza kuamini, lakini inahusu kile kitakachokuwa mji wetu wa nyumbani, mji wetu, nyumbani kwetu!

   Kumiliki Vitu vya Mungu Ambavyo Vimetolewa kwa ajili ya Wana wa Mungu

 

Hatutafurahishwa na fungu hili vile inavyotakikana hadi tujadili hoja hii muhimu: wakati umeshirikishwa kwa kitu kikubwa, miliki hicho kitu. Ni chako pia. Yeshua hasa alipaita mahali alikuwa akienda kuandaa kuwa “mahali penu”- “mahali pako.” Ni mahali petu. Ni yetu. Nataka hiyo izame ndani.

Wakati wowote unapochukua umiliki wa kitu, inamaanisha mengi zaidi kwako. Nyumba unayonunua inaonyesha “fahari ya umiliki” kwa jinsi unavyoitunza. Pamoja na gari unalomiliki dhidi ya gari umelikomboa. Unawapenda kuwajali Watoto wako dhidi ya watoto wa wengine. Familia yako dhidi ya familia za wengine. Kupalilia bustani ya mtu mwingine dhidi ya kupanda na kutunza bustani yako mwenyewe.

Yeshua anataka tuelewe kwamba atatutengenezea mahali. Baba anaelewa hili na anataka tutambue ufalme, mji, n.k. ni yake -lakini ametukabidhi haya pia. Navyo pia ni vyetu.

Hebu nieleze jambo hili kwa hadithi. Niliomba kijana yangu anisaidie na kazi ya uani na nilihitaji anikatie duara kandokando ya mti wa mcheri ambao niliupanda mwanzoni mwa mwaka, ili kwamba tupande maua chini yake au tupalilie ili tuondoe magugu. Alikuwa amechimba mduara mkubwa kuliko vile nilivyotarajia, lakini kwa kweli niliupenda. Nilimtajia kwamba ulikuwa mkubwa kuliko vile nilivyofikiria, kwa hiyo Jon mara hiyo akasema, “naweza rudisha nyasi na kuifanya iwe kiwango unachokiitaji.” Nikamwuliza, “Hiyo basi ni ya nini?” Jon: “ Kwa sababu ni nyumba yako.” Basi nikamwambia mwanangu, “Jon, hii ni nyumba yako pia. Ninaimiliki lakini unaishi hapa Pamoja nami, kwa hiyo ni yako pia.” Ningependa uhisi kwamba ni yako pia na kufanya uamuzi pia. Nafurahia kuona unacho kuja nacho.

Alionekana kufurahishwa na hilo. Nitaka achukue umiliki pia.

Kwa kweli, huu ni ufalme wake, Mwili wake, Kanisa lake. Lakini ikiwa tunaenda kuuchukuwa “Ufalme wa Mungu” kwa maanani, au “Kanisa la Mungu” kwa maanani, au “Bi arusi wa Kristo” kwa maanani, au Mwili wa Kristo kwa maanani, au hata, “ Ufalme wa Mbinguni” kwa maanani-uelewe kwa undani - umekuwa ndani

ya hayo yote ikiwa una Roho wa Mungu ( rudia) Tunazamishwa katika kila moja ya haya na Roho Wake Mtakatifu ( 1 Kor. 12:13). Mungu pia ni baba yetu, Mungu wetu. Daudi alimwita Yahweh “Mungu wake” tena na tena.

Ni ufalme wa Mungu, lakini pia ni ufalme wa Mwanawe. Je, unatambua hayo? Hakika, Mwana pia ni Mungu ( Yohana 1:1-3), lakini hebu tuelewe hili wazi:

Iliyo wazi sana ni Waef. 5:5, “…aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.”

Katika Luka 22:29—Yeshua anasema “Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi”.

Ndiyo, Yesu ana ufalme: Unaitwa ufalme wa Mwana katika sehemu nyingi, bila shaka katika Mathayo 16:28, Mat. 13:41, n.k.

Ni wazi: ufalme wa Mungu pia ni ufalme wa Masihi-na umehifadhiwa kwetu sisi tulio na Roho Wake, na tulio na mwili wake, au tulio ndugu na dada zake. Kumbuka sisi ni warithi wa vitu vyote Pamoja na Kristo ( Warumi 8:17; Wagal. 3:29). Haya yote yanawezekana ikiwa “tumo ndani yake”. Hayo si yanashangaza? Hiyo ina maana ufalme ni wako na wangu pia. Amini na ukubali.

Kwa hiyo ikiwa ufalme ni wa Yeshua pia, na ametufanya warithi Pamoja naye, na sisi ni wana wa ufalme basi-hiyo inatuambia nini?

Hata Hivyo: Kumbuka naenda nyuma na mbele nikitumia jina la Kiyunani-Kiingereza Yesu na jina la Kiebrania- Yeshua. Pia ninabadilisha neno la Kiyunani Kristo (mtiwa mafuta) na Masihi kwa Kiebrania-Kiingereza (mtiwa mafuta). Na mara nyingi mimi hutumia jina la kibinafsi la Mungu-Yahweh.

Kwa hiyo Masihi pia alisema sisi ni warithi Pamoja naye. Ikiwa mimi ni mrithi kwa kile ambacho nimehifadhiwa kwa ajili yangu, hiyo ina maana kwamba ni changu pia. Katika Waefeso 2:6-7, Paulo anasema tumeinuliwa na kukaa kiroho Pamoja naye kwa kiti chake cha enzi. Hatupaswi kuyapuuzia mafungu haya! Nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme, lakini “ ninyi hamfuati mwili, bali mwaifuata roho’ ( Warumi 8:9), na miili yetu ni NYUMBA tu, inayohifadhi mimi halisi na wewe halisi -roho iliyo ndani ya mwanadamu na roho ya Mungu ambayo ni wewe halisi!

2 Wakorintho 5:1-5

Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii, hema hii (mwili wetu) ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono [ufufuo wa mwili wa kiroho], iliyo ya milele mbinguni. 2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 3 ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 4 Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.

5 Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho.[ Kigiriki ya arabuni: arrabon. Kigiriki ya kisasa “ Arrabona”=pete ya uchumba.]

“Wewe halisi” na “mimi halisi” ni   roho!   Ninyi si wa mwili bali ni wa roho ( War. 8:9)- hata kama tuko katika mwili huu. Hivyo ndivyo jinsi sisi ambao ni nyama na damu wanaokufa twaweza kuwa “ Roho mmoja pamoja na Kristo” ambaye ni Adamu wa   pili ( 1 Wakor. 6:17). Kumbuka kwamba Adamu na Hawa walipaswa kuwa mwili mmoja. Tumeunganishwa na Mwalimu kwa Roho hiyo mmoja, akitufanya kuwa Roho mmoja pamoja Naye. Sisi ni sehemu yake, kwa hivyo sisi ni sehemu ya “mwili wa Kristo

Kidole gumba changu, kama kingeweza kuzungumza, kingechukulia mwili ambao ni sehemu yake, kama mwili wa “wetu” au “wangu” kama kingezumza. Mwili wa Kristo, kwa kuwa sisi ni viungo vyake, pia ni mwili wetu. Sisi ni sehemu yake (Warumi 12:4-5). Chukua umiliki wa mwili huu. Chukua hatua fulani wa umiliki. Itakuwa na maana zaidi, itakuhamasisha na kukusisimua.

Wakati wa kuandaa muunganisho wa chuo kikuu hivi majuzi na timu iliyojitolea, nilisisitiza kwa timu yetu kwamba haukuwa “muungano” lakini nilitakatuurejelee kila mara kama “muungano wenu”. Tulitaka kila mtu darasani ajisikie kama sehemu ya upangaji huo na kuuzingatia kuwa wao wenyewe. Yahweh pia anatutaka tuzingatie karama zake na vitu anavyotupa, na vile ambavyo ametufanya kuwa sehemu yake, kama vyetu sasa pia. Tena umiliki huifanya kuwa halisi zaidi nay a kusisimua zaidi kwetu.

Kwa hivyo yote hayo yanamaanisha nini? Ina maana kwamba sio “ ufalme” tu lakini pia ni ufalme wa wangu na wako. Sisi ni mabalozi wa Kristo na wa ufalme wake. Hiyo ina maana kwamba twapaswa kuwa tayari raia wa ufalme huo! Na ujue kwamba watoto ambao hawajazaliwa sio raia wa kitu chochote bado. Paulo anasema kwamba sisi ni wenyeji Pamoja na watakatifu na tayari tu washirika wa nyumba ya Mungu. ( Waefeso 2:19). Paulo anaongea kwa wakati uliopo kuhusu uhusiano wetu na ufalme wa Mungu, ambao pia ni ufalme wetu.

Najua kwamba hatuhisi kwamba tuko katika ufalme bado-lakini hilo ndilo Paulo analinena katika 2 Kor. 5:3. Lakini tunachohisi na hakika ni vitu viwili tofauti! Najua haya yanaenda dhidi ya yale ambayo wengine wetu tumefundishwa, lakini tutafanyaje? Ng’oa mafungu ambayo yameeleza waziwazi kuhusu haya niliyonena? Na pengine twapaswa kuamini na kuhisi ufalme Zaidi.

Hata hivyo, kwa hiyo tunapaswa kuliita kanisa la Mungu, kanisa letu. Mimi ni wa Mpendwa na Mpendwa ni wangu ( Wimbo Ulio Bora 2:16; 6:3). Mimi ni wa Mungu- na yeye ni wangu, na kwa hivyo namtaja Mungu kama “ Mungu wangu”, kama vile manabii wa zamani. Zaburi zimejaa Daudi kumwita Yahweh “Mungu wangu.” Utazame katika Konkodansi. Pia uangalie neno, “Baba wetu”. Hata tunaambiwa tuombe “ Baba Yetu aliye mbinguni…” Ukishika wazo hilo, utakuwa mbele ya wengi.

Katika “ Agano la kale”, neno “the” halipatikani kwa Kiebrania la awali ambayo unasoma kwa kiingereza “ the LORD” yaani BWANA. Katika lugha ya Kiebrania ni “ Yahweh”, bila hilo neno “the” la kiingereza. Hata mara nyingi nasema tu, “Abba” au “ Baba” badala ya kutumia “the” ya kiingereza.

Thiolojia yangu inaweza kujumuishwa na yule niliye sehemu yake- na yule aliye baba yangu-ambaye ni Mungu wangu.Hiyo ndiyo Eliya aliwafanya Israeli wakutane nayo: mtamwomba nani? Mungu wa kipagani ambaye haishi na anayeitwa Baali, au Yahweh wa milele! ? Kwa hiyo thiolojia yangu yaweza kujumuishwa kwa maneno manne: “ Baba yetu aliye mbinguni…” Kwangu, hiyo inaeleza yote tukielewa anachofanya Baba yetu. Mungu anatueleza kwamba anataka awe Mungu wetu. Yeye siye tu Baba lakini ni Baba yetu.Hiyo pia ndio maana Daudi anarudiarudia kuhusu “ Mungu wangu” katika Zaburi. Mimi ni wake na yeye ni wangu. Kwa kweli utakuwa ni wakati wa UTUKUFU ambapo inaweza kusemwa juu ya Israeli wote. utakaponenwa kwa Israeli, “ nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu” ( Kut. 6:7). Yahweh alimwambia Ibrahimu kwamba anasubiri wakati ambapo “ nitakuwa Mungu wao”

(Mwanzo 17:8).

Kanisa pia ni “langu” na lako. Twasukuma hiyo kwa sababu inaonekana kuwa ni dhambi. Lakini sisi ni sehemu ya mwili wa Kristo, sehemu ya Kanisa la Mungu, kwa hiyo ni mwili wetu wenyewe, kundi letu, familia yetu. Fanya kuwa yako. Silo kanisa linaloongozwa na binadamu tu, japo wengine wanajifanya kana kwamba kundi ni lao badala ya kuwa wachungaji wadogo chini ya

Mchungaji

Mkuu. Kanisa, kundi lililoitwa, ni kundi lake, na siku moja atawakusanya Watoto wa Mungu wote ambao wametawanyika ( Yohana 11:49-52) katika zizi moja, kundi moja ( Yohana 10:16). Huo ndio umekuwa ujumbe wangu kwa siku nyingi hadi leo.

Kwa hivyo mahali hapa ambapo pameandaliwa ni pako na pangu. Je, hatuwezi kusema ni “mahali pako” ni sawa na “sehemu yako”?

Hoja ya haya yote: Chukua umiliki. Ni yako kiasi. Umo ndani yake. Amini. Tenda kama io.

SAWA, hebu turudi nyuma na tuanze na pendekezo la harusi kisha tuende mpaka kwenye harusi yenyewe. Naongea kuhusu haya Siku ya Pentekoste mara nyingine tena, kwa sababu Pentekoste ndio wakati Mungu alimwoa Israeli. Pentekoste ilikuwa ndiyo wakati Boazi, mfano wa Kristo, alimwoa Ruthu, mfano wa Kanisa. Pentekoste kama ninavyohisi ndio wakati ambapo karamu ya harusi ilifanywa…na kisha tutarudi duniani na Mume wetu mpya kwa wakati wa Sikukuu za mavuno na kukanyaga Mlima wa Mizeituni. Wahudumu wengi wengi mno wananena juu ya hili na wako tayari kusema ndivyo wanaamini.

PENDEKEZO la Harusi

Kwa hali nyingi, majadiliano kuhusu nani aliyeoa nani yalifanywa kati ya baba wawili: baba wa Bwana Harusi na baba wa Bi Harusi. Bwana na Bi arusi hawakuwa na mengi ya kusema. Hiyo ndiyo hali iliyoko katika nchi za mashariki hadi leo.Twaona haya katika mifano mingi ya Biblia. Hata wakati mtumwa wa Ibrahimu alipoenda kumtafutia Isaka mchumba, alijadiliana na Bethueli, baba wa Rebeka, kuliko Rebeka mwenyewe, japo Rebeka alikuwa na kauli mwishowe. Lakini Isaka hakumchagua Rebeka; mtumwa wa babake Isaka alifanya hayo.

Kiroho, Mume wetu Yeshua hakuchagua sana kama Baba yake alivyochagua. Ni Baba wa mbinguni ndiye anayetuchagua wale wanaoitwa kuwa Bi arusi wa Masihi (Yohana 6:44-45, 65).

Yohana 6:45.65

44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho.

45 Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu. 65 Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu. "

Je, umewahi kujiona kwamba wewe si mtu? Au kwamba mtu yeyote wa maana anayekujua? Hatupaswi kuwa na fikra hiyo kwa sababu hauchaguliwa na mtu yeyote pasi na Mungu aliye juu. Ndio, wewe! Kisha twaletwa kwa Mwana, ambaye anatufunulia Baba yetu mpya (Luka 10:21). Lakini aliye juu sana katika ulimwengu wote alikuchagua. Kibinafsi na kipekee. Baada ya kuitwa, tunapaswa kuitika na kukubali wito, kama vile Rebeka alivyofanya. Wengi wameitwa, wachache wamechaguliwa, lakini tunapaswa kuitika na kutii.

Kununuliwa na Kukombolewa

Bi arusi alinunuliwa na bei ya “ kuposwa” au bei inayoitwa “ Mohar” kwa Kiebrania. Babake Bi arusi ndiye aliamua gharama ya kulipwa. Wengi wenu hamtapenda hili, lakini kabla hatujakuwa Watoto wa Mungu, tulikuwa Watoto wa mwingine! Tazama Yohana 8:44-47. Nyoka ana uzao wake mwenyewe ( Mwanzo 3:15). Kaini alikuwa “mtoto wa yule mwovu” ( 1 Yohana 3:12). Je, unashika mkondo wangu? Hiyo pia ndiyo sababu pia Shetani aliweza kutoa falme kwa Masihi katika Mat. 4.

Yohana 8:44, 47

44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda ….

47 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

Kwa hivyo tulimilikiwa na mungu wa ulimwengu huu (2 Kor. 4:4) na tulipaswa kukombolewa (kununuliwa na kulipiwa) kwa damu ya Mwana - Kondoo, Mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo gharama ya kununuliwa. Hatukukombolewa au kunuliwa na vitu vinavyoharibika bali kwa damu ya Masihi ( 1 Pet. 1:17-19). Hiyo ndiyo ilitufanya tuwe wake 1 Kor. 6:20 inasema “mlinunuliwa kwa thamani”, na kwa hiyo tunapaswa kumtukuza Mungu katika miili na roho zetu ambazo sasa ni mali ya Mungu.

Ni Nani Aliye Bi Arusi wa Kristo?

Bibi arusi ni nani? Tumefundisha mara nyingi kuhusu- wale wanaoitwa kutoka kwa ulimwengu. Hawapaswi kupatikana katika dhehebu au shirika lolote, kwa sababu Mungu hawezi kupangwa. Bibi arusi ni Kanisa, mwili wa Kristo-kama vile ilivyoonyeshwa katika Kol. 1:15-18’ Waefeso. 1:22-23. Sisi ni kama bikira aliyeposwa kwa Masihi—Waefeso. 5:23-24, 2 Kor. 11:2.

Mara baada ya Bwana Arusi kulipa mohar, maelewano ya ndoa au agano liliimarishwa, lakini kwanza Bi Arusi lazima akubali kuolewa na Bwana Arusi. Je, twaweza kusema ilimbidi kukubali mwaliko wa arusi na wito, kama tunavyopaswa kufanya ? Ndivyo ilivyo. Mfano mzuri ni Rebeka ambaye angekubali kwanza kuenda na mtumishi wa Ibrahimu ( Mwa. 24:57). Tumeitwa, lakini tunapaswa kuitikia wito ili tuwe Bibi Arusi wa Kristo na kuhudhuria karamu ya harusi.

Kuposwa kulikuwa Zaidi ya “uchumba” wa siku hizi. Ili uvunje ndoa hiyo, mwanamume lazima angepeana talaka, kama vile tunavyosoma kuhusu Yusufu na Mariamu. Wakati Yusufu alikuwa akidhani kwamba Mariamu sio mwaminifu, alikuwa akifikiria kumpa talaka ( Mathayo 1:19) hata hivyo hawakuwa wameoana. Talaka ingefanywa ili gharama ya kupoza ingerudishwa ili awe mwanamwali tena.

Kikombe

Kuthibitisha maelewano ya uchumba, atakayekuwa Bi arusi na Bwana arusi wanakunywa kutoka kwa kikombe cha divai cha bwana arusi, hiyo inaonyesha kwamba yu tayari kupitia maisha na huyu bwana bila kujali kilicho ndani ya “ kikombe chake”. Kikombe kinaonyesha kinachowasubiri mbeleni. Kumbuka wakati Yeshua alilia kule Gethsemane kuwa ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke? Kukunywa kwa hicho kikombe kilimaanisha kukubali chochote kile kitakachotokea katika maisha yao wakiwa Pamoja, alikuwa akikubali “ iwe nzuri iwe mbaya.”

Hili ndilo Yeshua alisema katika ( Mathayo 26:27-29) kwa wanafunzi wake wakati wa chakula cha mwisho cha jioni! Hakika alikuwa akitengeneza mkataba mpya, pendekezo la ndoa, na washirika wa kwamza wa Kanisa lake.

Mathayo 26:27-28

“27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;

28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi."

Alikuwa akiwapendekezea, na kuwapa agano la ndoa. Na wakati tunakunywa kikombe cha Pasaka, hatukubali tu damu yake juu yetu, lakini pia kukubali kupokea kile ambacho Mungu ametuhifadhia hadi kurudi kwake.

Bwana Harusi basi ataenda nyumbani mwa baba yake na kuahidi kwamba atarudi na kumchukuwa bi arusi nyumbani baada ya kuwa tayari. Hiyo ndiyo tulisoma awali-katika Yohana 14:1-3.

Naamini kwa uthabiti kwamba ndiyo, tunaenda mbinguni kufunga ndoa na harusi itafanywa mbinguni. Sijui vile utakavyosoma Sura za Ufu. 14, 15, 19 bila kuyaona hayo. Tutarejea kwa hili baadaye katika mahubiri. Huo ndio mji wetu, nyumbani kwetu, japo tutatawala duniani kwa miaka elfu.

Ninaamini mbingu ni thawabu ya waliookolewa, ingawa mbingu zinakuja kwenye dunia mpya nasi tutafanya hivyo siku moja kuishi “mbinguni duniani”. Wakati yote yamesemwa na kufanywa. Tutaenda mbinguni baada ya kufufuka kuaolewa na baadaye kurudi duniani kufanya kazi, lakini NYUMBANI kwetu itakuwa Yerusalemu ya mbinguni na Abba Baba yetu.

KAZI yetu itakuwa hapa duniani. Nyumbani kwetu itakuwa katika Yerusalemu ya mbinguni. Mbinguni ndiyo nyumbani kwetu, mji wetu, nchi yetu. Na hiyo ndiyo yamenenwa na maandiko kila mara.

Japo nimefundisha kwa miaka na mikaka kwamba tunaenda mbinguni kuolewa, Nilisikia maelezo mazuri ya “ umilikaji” katika mahubiri ya Jeff Niccum aliyotoa miaka mingi iliyopita. Jambo aliloweka wazi Jeff katika yale mahubiri yake ni dhana kwamba Yerusalemu ya mbinguni ni mji wetu. Ndio mji wa Bi arusi, na ndio maana unaitwa “ Bi arusi” katika Ufu. 21-22.

Lakini nazidi kuendelea mbele. Tukirejelea wakati ule wa kupozwa.

KUJITAYARISHA kwa Arusi

Siku na Saa haijulikani

Kinyume na harusi zetu za kisasa za magharibi ambapo terehe ya harusi, wakati, maneno na mealezo yote yanajulikana na kufichuliwa miezi kadhaa kabla, hapo zamani ilikuwa tofauti.

Bwana arusi-hata Yeshua! -hakujua tarehe kamili ya kurudi kwake kumchukua Bibi –arusi kwa ajili ya harusi (Mathayo 24:36). Hiyo ilikuwa jukumu la Baba, ambaye alikuwa anaamua wakati ambapo Bwana arusi ametayarisha vilivyo mahali pa Bi arusi. Wakati mwingine katika familia maskini sana, ilikuwa ni nyongeza kwa nyumba ya baba. Wakati mwingine, kulikuwa na kao tofauti.

Kwa hiyo Bi arusi angejua wakati wa arusi unapokaribia, lakini hakujua siku wala saa ( Mathayo 24:36; 25:13). Lakini Bi arusi hawezi akapatikana kama hajawa tayari. Fungua 1 Wathes. 5:1-5 ambapo kurudi kwake kumelinganishwa na uja uzito. Katika uja uzito, tunayo siku kamili. Mama mjamzito huandaa mikoba yake tayari ili aitikie haraka. Anajua kwamba wakati unakaribia, lakini si siku au saa. Lakini pia haipaswi kuwa ya mshangao sana inapofanyika

1 Wathesalonike 5:1-5

Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. 4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. 5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.

Wakati Bwana arusi amerudi, alikuja kumleta Bi arusi nyumbani. Hii kawaida ilifanyika usiku. Bibi-harusi wakati huo huo alikuwa akiandaa vitu vyake, kitani chake na kujitayarisha kuwa bibi arusi aliye tayari kwa ajili ya harusi yake. Pia aliwakusanya wahudumu wake, ambao katika siku za Biblia kiajabu walikuwa wanawali kumi. Tazama Mathayo 25

Wanawali 10 ni kina Nani?

Katika Mathayo 25:1-13 inaongea juu ya wanawali kumi. Haiongei juu ya Bi arusi 10. Nimesikia Mat. 25 ikitumiwa kueleza juu ya kanisa. Je, hii ni sahihi? Nasema kwamba andiko hili halisemi “Bi arusi”, linasema “ mabikira”- wahudumu wa Bi arusi.

Mabishano ya kusema kwamba wanawali 10 ni Bi arusi:

  • Bi arusi wa Kristo pia anaonyeshwa kama bikira (2 11:2).
  • Malimbuko ya kwanza 144,000 waliokombolewa katika 14:1-4 wameelezwa kama mabikira ambao wanamfuata Mwana Kondoo mahali popote aendapo. Je, huyo ni bikira mmoja – au 144,000 ingawa?
  • Ukweli kwamba wanawali wote kumi wanalala ni sawa na maonyo mengi kwa kanisa kutolala.
  • Kama hawa 10 sio Bi arusi ( ukweli ni Kwamba 5 ndio walipata kuingia), basi wao ni kina nani?

Majadiliano yanayotumika kusema kwamba wanawali kumi sio Bi arusi:

  • Hakuna mahali hawa wanawali wanaitwa “Bi arusi”. Lilikuwa jambo la kawaida kwa maharusi kuwa na wahudumu 10, mara nyingi ni wasichana wadogo, ambao walimsaidia na kumsindikiza Bi arusi. Je, hawa kumi pia wanaweza kuwa wasaidizi, kama vile Rebeka alikuwa na wajakazi ambao walimsindikiza kwa Isaka?
  • Kristo anakuja kuoa bikira mmoja, mwili mmoja – sio kumi.
  • Zaburi 45:13-15 inazungumnza juu ya wanawali pamoja na Bi- arusi katika kasri.

13 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu, Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu. 14 Atapelekwa kwa mfalme Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri. Wanawali wenzake wanaomfuata, Watapelekwa kwako. 15 Watapelekwa kwa furaha na shangwe, Na kuingia katika nyumba ya mfalme.

Naleta haya ili uzingatie. Andiko linaloongea juu ya karamu ya arusi ambapo tuna Mfalme, Bwana Arusi pamoja na wageni/ wanageni na wahudumu wa harusi ni akina nani? Je, wao pia wanapatikana katika ufufuo wa kwanza?

Inawezekana kwamba wengine wanaopatikana katika ufufuo wa kwanza ni Bibi-harusi na wengine ni wahudumu? Sijui. Hakika sijui. Lakini naleta hii ili ifanye kazi kwa njia hiyo. Pengine uelewa wetu wa ufufuo, na wale watakaokuwa kwa huo ufufuo, unahitaji marekebisho fulani. Tumekuwa tukidhani hapo awali kwamba wale walio wa Bi arusi ndio watakaokuwa katika ufufuo wa kwanza. Huenda niliwahi kusema hivyo hapo awali. Sina uhakika kulingana na maandiko yale ninayoyaleta hapa; maandiko ambayo yameniduwaza kwa miaka mingi. Hili silo fundisho la wokovu, lakini ni jambo la kuwaletea hamu ili kwamba tuwe na taswira Zaidi ya vile tumedhani hapo mwanzo.

Nadhani kwamba kuna uwezekano kuwa ufufuo wa kwanza utajumuisha wale walio wa Bibi arusi , na pia wahudumu wa Bibi arusi, na wale ambao ni wageni katika arusi-ila tu kama hawa wahudumu na wageni watakuwa malaika. Jaribu kujipa kiini kwa mambo ya kiunabii

Hata hivyo ,wacha tusome tena fungu jingine ambalo tulisoma awali! Angalia Luka 12:35-38 na wakati unapoonyeshwa hapa. Katiza sauti kwa dakika moja ili upate kuelewa kile ambacho mafungu yanasema..

Luka 12:35-38

" 35 Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. 37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia. 38 Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao..”

Nilidhani kwamba Kristo anatupeleka arusini na tunapaswa kuwa tayari kuenda arusini. Na hapa anasema atatoka arusini na tuwe tukimgoja atakaporudi KUTOKA arusini. Je, umewahi kutambua jambo hili? Hili linamaanisha nini? Je, kuna uwezekano kwamba arusi imeshaandaliwa. Masihi yuko arusini, na baadaye atarudi kumleta Bibi arusi kwa arusi ambayo iko tayari kuanza? Je, ndivyo inavyosema? Najaribu kutaja kwamba vile maneno yamewekwa hapa, ukichunguza kwa makini, ni ya kushangaza.

Hata hivyo, turudi kwa Mathayo 25 na wale wanawali 10. Katika harusi za siku hizo, KARAMU ya kawaida ya harusi, KUNDI la watu walikuwa wakiondoka pamoja na Bwana arusi wakienda nyumbani kwa Bibi arusi. Naye akarudi na Bwana harusi tena, katika kikundi. Haikuwa Bibi- arusi na Bwana harusi tu. Ilikuwa ni watu wengi. Bwana harusi alikuwa na watumwa na wasidizi na marafiki. Jambo hilo hilo wakati Kristo anarudi kutakuwa na mamilioni ya mamilioni.

Mathayo 25:1-5

“Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi..”

Kumbuka kwamba japo 5 juu ya 10 wanaitwa “wenye busara”, WOTE walilala. Je, BIBI ARUSI pia alilala? Inasema hapa “wanawali” -sio Bibi Arusi.

Je, Mathayo 25 inaongea juu ya Bibi Arusi wa Kristo? Yuawezakuwa kwa sababu Bibi Arusi mara nyingi ameonyeshwa kama mwanamwali/bikira katika sehemu nyingi ( 2 Kor.11:1-2). Katika Ufu. 14-15, Bibi arusi ameonyeshwa kama wanawali. Lakini tena usisahau Zab. 45 niliyosoma awali, ambayo inaongea juu ya “ wanawali.”

Pia katika Mathayo 22:9-10, inaongea juu ya “ wageni” walio karamuni-ambao wamealikwa na Mfalme kwa ajili ya Mwanawe. Bibi arusi sio mgeni. Haiongei juu ya Bibi Arusi. Wageni hawa ni kina nani? Wahudumu hawa ni kina nani? Tutasubiri na kuona.

Je, hili laweza kuwa halizungumzi kuhusu Bibi Arusi mwenyewe, kama vile tulivyokwisha kufundishwa? Wanawali ni kina nani? Je, twawezasema kwa hakika kwamba wale wanawali kumi wanawakilisha kanisa, Bibi Arusi?* Neno “Bi arusi” halijatajwa hapa, kama vile lilivyotajwa katika Ufu. 19, kwa mfano.

Kumbuka hili: Kristo anaoa mwili MMOJA, sio kumi! Bikira MMOJA, kanisa, siyo makanisa kumi. Haya ndiyo nayafikiria kwa wakati huu. Nadhani hili ndilo lilionyeshwa na Adamu alipopewa mke MMOJA, sio wake wengi. Ilikuwa Adamu na Hawa, sio Adamu na Hawa, Mariamu, na Abigaili! Baada ya kusema hayo, bado natambua   kwamba watu wengi wanaweza kuonekana kama “ mwili mmoja” Kibiblia. Nasema tu kwamba-kubali matukio mengine ili kwamba usipate kushangaa. Kwa hiyo Mathayo 25 inaweza kuhusu Bibi arusi, au kuhusu wahudumu wa Bibi arusi

Katika Mathayo 25:3-wapumbavu “hawakutwaa mafuta” kama ilivyonenwa, lakini katika mstari wa 8, wapumbavu watano walisema taa zao “zinazimika” (au KJV “zimezimika”). Kwa hiyo walikuwa na mafuta lakini hayakutosha kwenda mbali! Maneno ya “kuzimika” ni sawa na neno la “kuzimisha” kama katika 1 Wathesalonike 5:19, “Msimzimishe Roho”. Kwa hiyo walikuwa wakifanya mambo ambayo yalikuwa yakimzima Roho Mtakatifu. Hiyo inafaa kujifunzwa pia, sivyo?

Pia kumbuka kwamba Yesu Mwenyewe katika mfano wake anaeleza katika mstari wa 5, “ Hata Bwana arusi alipokawia…” Unaelewaje hilo?

Mathayo 25:1-10

"1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. 3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; 4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. 6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. 7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. 10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

Kumbuka kwamba wanawali 5 sio wachoyo kwa kukosa kupeana mafuta. Hatuwezi kupeana uhusiano wetu na Baba kwa mwingine. Hilo ni jambo ambalo kila mmoja wetu lazima alitende. Andiko linasema kwamba katika wakati huu wa mwisho, sio hata Nuhu, Danieli au Ayubu angeweza kuokoa ye yote ( Ezekieli 14:14-16. 20: tazama Yeremia 15:1). Kuwa tu “ndani yake” ndio itakuokoa mwishowe. Tunapaswa kuenda kwa chanzo cha “mafuta” sisi wenyewe. Hakuna mtu atakayetufanyia. Tazama pia Ufu. 3:17-18 kwa Walaodikia.

Isaya 55:1

Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.

Kelele

Wakati Bwana arusi alipofika, kupeana taarifa mapema, kutakuwako na kelele, “ Haya bwana arusi!”- Kama vile Mathayo 25:6 inavyosema. Tulisoma hapo awali katika 1 Wathes. 4:16-17 jinsi Bwana anakuja kwa KELELE, pamoja na sauti ya malaika mkuu.

1 Wathes. 4:16-18

Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

Baadaye wanaenda pamoja sehemu tofauti kwa ajili ya arusi: nyumbani mwa Bwana arusi! Bibi arusi na wahudumu wake basi kwa kelele wataenda nyumbani kwa mposaji, wakiwa na mwangaza mwingi. Yeshua pia anarudi na mwangaza mwingi mno. Kuja kwake kutakuwa kama umeme umulikao juu ya anga, ambao utang’aa katika usiku wote ( Mathayo 24:47). Wakati anapokuja, itakuwa wazi sana,

amekuja! Hatutashangaa au kuchanganyikiwa na Yesu wa uongo wa siku za usoni wa Waislamu au mlaghai fulani atakayeonekana katika Dameski au jangwani akijidai kuwa Yesu wa Biblia

WANAENDA WAPI BAADAYE? Arusi Itafanyika Wapi?

Mathayo 22:1-14. Wacha tusome mstari wa 2:

2 Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi,”

Bwana arusi ni Mwana. Sasa twajua Mwana ni nani. Mfalme ni nani? Dhahiri ni Baba, Mungu aliye juu! Nani atakayetekeleza arusi? Inabidi niamini itakuwa Baba MWENYEWE, pengine mbele ya Bahari ya kioo! Tazama pia Mathayo 9:15, mahali ambapo Yesu alijifananisha na Bwana arusi. Yesu alienda wapi baada ya ufufuo wake? Kwa Baba Mbinguni. Yuko wapi sasa? Mbinguni. Baba wa Yesu Kristo yuko wapi? Mbinguni.

Mathayo 22:11 – “Alipoingia yule mfalme kuwatazama wageni….”

Kwa hivyo arusi inafanyika mahali Baba mwenyewe anajitambua mwenyewe kwa wageni. Baba yuko mbinguni na haji duniani hadi miaka elfu itimie-Ufu.21:1-4. Hakuna mtu ye yote aliyemwona Mungu Baba, kamwe ( Yohana 1:18; Yohana 4:12) ila tu Mwana Yeshua ( Yesu Kristo). Hakuna mtu awezaye kumwona Mungu Baba katika hali yake ya utukufu hadi binadamu abadilishwe kuwa roho na apate kuwa kama Mungu.

1 Yohana 3:1-2, katika muktadha wa Mungu Baba.

Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa ( BABA!), tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo(BABA!).

Kwa hiyo Mungu aliye juu, Mungu Baba, anajidhirisha mwenyewe kwa Bibi-arusi kwenye arusi. Lakini ni aliyetupeleka huko? Kwa njia gani twaweza kuwa katika uwepo wa Baba? Ni kwa kurudi pale na Mwana wa Mungu. YEYE ndiye Njia, Uzima. Hakuna njia yoyote ya kufika kwa Baba, hata kihalisi.

Basi kumbuka mahali ambapo Mungu yuaishi. Hata tunaomba’ “ Baba yetu uliye mbinguni…” Mat. 6:9

Waebrania 12:22-24

22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, 23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, 24 na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

Basi pia kumbuka pia Yesu alisema, “ Naende kuwaandalia mahali.” Mji wetu ni upi? Kumbuka nilivyosema kuhusu umilikaji hapo awali? Yerusalemu ya mbinguni sio tu mji wa Mungu; bali ni mji wetu, tuliohifadhiwa sisi ambao tumesajiliwa mbinguni.

Waebrania13:14 inasema, “.Hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao” Mji WETU ni ule ulio juu.Ibrahimu alijua hivyo, kina baba wote wa Imani walijua hivyo:

Waebrania 11:9-10

9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

Waebrania 11:16

Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

(Inaonekana kama “Naenda kuwaandalia mahali.” – Yohana 14:1-3)

Kuna mengi. Mengi Zaidi, ya kuonyesha kwamba tunaenda mbinguni kuolewa na kwamba Yerusalemu yote ya kibingu ni mji wa Bibi arusi! Kutakuwako miji mingi, lakini Bibi arusi ataishi katika Yerusalemu ya mbinguni.

Kumbuka kwamba Waliokombolewa hata wana jina la mji huo umebandikwa kwenye paji ya nyuso zao. Pengine hata kwa taji au kwa njia nyingine? Au pengine imebandikwa kwa njia ya kawaida kwenye vipaji vya nyuso zao.

Ufunuo 3:12

“Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.

Hii ndiyo maana Paulo alisema kwamba tayari sisi ni mabalozi wa mji huo na raia wa mji huo! Kwa sababu hiyo ni “ nchi yetu”, “ mji wetu”! (Wafilipi 3:20).

Hiyo ndio maana Ufu. 21:2, 9-10 unaita mji wa Yerusalemu mpya kama “Bibi arusi”. Mji huo una uhusiano wa karibu sana na Kanisa (Bibi arusi wa Kristo), kiasi kwamba mji wenyewe unaitwa Bibi arusi. Pengine hili linafanya kwa njia sawa na vyombo vya habari ambavyo vinarejelea Washington DC kama uongozi wa Marekani. Twaweza soma taarifa kama “Washington DC inasema…

Kuna mengi ya kuthibitisha hili jambo. Wakati Ibrahimu-ambaye alikuwa ni mfano wa Mungu Baba-alipomtuma mtumishi kuchukua Bibi –arusi kwa Isaka (mfano wa Kristo), mtumishi alienda kwa familia. Tunapaswa kuwa sehemu ya familia ya Mungu pia. Alimpata Rebeka akiwa kwenye vidimbwi vya maji vilvyo hai, kama vile Matendo 2 na Roho Mtakatifu. Mtumishi alimleta Rebeka kwa Isaka (kama vile malaika watatusanya toka kwenye pepo nne na kutuchukua kwa Masihi)…ambaye sasa alifanya nini? Ina maana MINGI.

HEMA LA SARA

Mwanzo 24:61-67

61 Rebeka akaondoka na vijakazi wake, nao wakapanda juu ya ngamia, wakamfuata yule mtu. Naye huyo mtumishi akamchukua Rebeka akaenda zake. 62 Basi Isaka alikuwa amekuja kwa njia ya Beer-lahai-roi, maana alikaa katika nchi ya kusini. 63 Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja. 64 Rebeka akainua macho, naye alipomwona Isaka, alishuka juu ya ngamia. 65 Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki?

Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika. 66 Yule mtumishi akamwambia Isaka mambo yote aliyoyatenda.

67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake.

Ikiwa hii inaonyesha arusi ya kanisa na Mesia, basi Sara nah ema yake inaonyesha nini?

Wagalatia 4:23-27

Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana [Sara] kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi [katika mukhutadha, inaashiria Sarah ambaye ni mwanamke huru”]. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume.

Yerusalemu ya juu ni mama yetu sisi sote. Tunachukuliwa kuwa tulizaliwa katika Yerusalemu ya Mbinguni.

Zaburi 87:4-6

Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo.

5 Naam, mintarafu Sayuni itasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye juu Ataufanya imara.

6 Yawheh ( BWANA) atahesabu, awaandikapo mataifa, Huyu alizaliwa humo.: [kumbuka Waeb. 12:23- wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni]

"Huyu alizaliwa huko."

   Hivyo ndivyo unazaliwa kiasili kuwa raia wa nchi yoyote-kwa kuzaliwa hapo

Mara baada ya kufika nyumbani kwa babake Bwana -harusi, Bi arusi na Bwana arusi wangeingia katika Huppah (tahajia ya sherehe, Kiebrania chuppah), chumba cha Bi arusi, mahali ambapo wangefunga ndoa yao na zingedumu kwa siku 7.

. Lakini BI ARUSI ANABAKI AKIFICHWA ndani ya huppah, chumba cha arusi, wakati huo

Nilitoa mahubiri awali-mnamo mwaka wa 2004. Ninaamini kwa sehemu tatu ya mahubiri mfululizo “Siri ya Kristo na Kanisa”. Katika Sehemu ya 3, iliyotolewa MACHI 2004, niliandika kwa ufasaha jinsi waweza kuona hekalu la mbinguni limefunguliwa, kasha kufungwa, baadaye kufunguliwa tena. Wakati wa kufungwa ndio wakati naamini arusi inaendelea humo ndani. Imechambuliwa kwa kina katika nusu ya sehemu ya mahubiri hayo. Tafadhali yaangalie.

Kwa kifupi ni hivi:

  • Ufufuo unafanyika wakati wa baragumu ya mwisho. Kuna baragumu 7, kwa hivyo labda ya 7 ndio tarumbeta ya mwisho, lakini kuna wengine wanabishana kuhusu hoja hii. Ninasema ni ya 7/ Ufu. 11:15 inanena juu ya baragumu ya mwisho kisha baadaye ufufuo unafanyika.
  • 11:19 – hekalu la mbinguni linafunguliwa na kasha kufungwa wakati wa mapigo 7 ya mwisho.
  • 12-13 ni mafungu ya ndani.
  • 14:3 inaonyesha watakatifu wakiwa mbinguni kwenye bahari ya kioo mbele ya kiti cha enzi. Hii ni baada ya ufufuo, baada ya tarumbeta ya 7 ya Ufu. 11:15. Sehemu iliyobaki ya surs ya 14 inaonyesha malaika wakaja na kuondoka. Muktadha umeonyeshwa wazi ni mbinguni. Jisomee mwenyewe.
  • Ufunuo 15:1-6-soma peke yako-tena muktadha uko MBINGUNI. Watakatifu washindi wanasemekana kuwa wamesimama kwenye bahari ya kioo ( 15:2) na kuimba. 15:5-hekalu limefunguliwa. Kisha malaika 7 wa mapigo 7 ya mwisho wanajitokeza ( mst.6). Inazungumnza juu ya wale viumbe hai wanne –hiyo ni wazi mbinguni pia.
  • Ufunuo 15:8-hakuna mtu ye yote aliruhusiwa kuingia hekaluni hadi mapigo saba yafanyike. Inaonekana watu 144,000 wamo hekaluni. Wakifanya nini? Huenda ikawa tunaonekana ana kwa ana na Abba. Pengine twapokea majina yetu mapya. Au pengine twapokea ujira wetu na maoni kutoka kwa Aliye Juu kabla ya arusi? Andiko halitaji kinachoendelea, lakini twajua mambo hayo yanatokea wakati fulani. Fahari, ukuu, mhemko, furaha itakuwa ya kupindukia.
  • Wakati tunapofika Ufunuo 19, arusi na karamu ya arusi, huko mbinguni itakuwa tayari kufanyika. Soma maneno katika Ufu. 19 kuhusu Arusi. Muktadha wote ni kule mbinguni, ukitutazama kwa uso. Hapo ndipo itafanyika! 19:1, 11, 14.

Wengine wetu wamekuwa wakihubiri kwa miaka mingi kwamba kama vile Mungu alivyowaona Israeli siku ya Pentekoste, analioa kanisa pia siku ya Pentekoste. Sijui siku atakayokuja kutufufua na kutupeleka nyumbani kwa Abba (Mungu Baba yetu), lakini inaoenekana arusi yenyewe itaanza siku ya Pentekoste na itachukuwa wakati fulani huku mapigo 7ya mwisho ya Ufu. 16 yakimiminwa. 

Warumi 7:1-8 inahusu jinsi baada ya Yesu kufa, Alikuwa huru kuoa Bibi arusi, wakati huu ni kanisa la kiroho, badala ya taifa la kawaida la Israeli. Kwa hiyo ninaamini kwamba Pentekoste pia inahusu arusi ya Bibi arusi wa Kristo kwa Mwana wa Mungu-na kwamba inafanyika katika mji wetu, mji wa Mungu, mji wa watakatifu-Yerusalemu ya mbinguni.

Ndiyo, tunarudi mbinguni kuoa. Yesu alimwambia Tomaso katika Yohana 14:5-6 kwamba afurahi kwa sababu anaenda kwa baba, na hakuna awezaye kuja kwa Baba bila kupitia kwa Yesu. Maana kuu ni kwamba Yeshua ndiye mlango (Yohana 10:1-5), njia pekee ya kufika kwa Baba. Kweli. Lakini hata kikawaida, akija kuchukua Bibi arusi wake, atataka kutupeleka moja kwa moja nyumbani kwa Abba, Baba yake na Baba yetu! 

Wengine wanapinga kusema harusi itafanyika siku ya Pentekoste kwa dhana kwamba kunafaa kuwa na sauti kubwa ya tarumbeta na hiyo inaonekana inafaa zaidi katika Sikuku ya Baragumu, wanasema hivyo. Lakini usisahau pia kulikuwa na mlio mkali sana wa tarumbeta siku ya Pentekoste kwenye Mlima Sinai wakati wa kutolewa kwa amri kumi ( Kut. 19:9; 20:14). Kwa hivyo, baragumu zinapigwa kila sikukuu.

Pia nitasema hivi: hata ikiwa arusi kamili haitafanyika siku ya Pentekoste, nahisi ni wazi kwamba arusi itafanyika, wakati itafanyika, huko mbinguni.

Kisha baada ya karamu ya arusi-pengine miezi mitatu ya dunia baadaye, Bibi arusi (watakatifu/kanisa, pamoja na malaika) wanarudi duniani kutua kwenye Mlima wa Mizeituni, hasa wakati wa Sikukuu ya Baragumu.

Wakati huu tunarudi kufanya vita na majeshi makubwa ya ulimwengu, yaliyokusanyika karibu na Yerusalemu hadi Galilaya-ambao wanapigana na Mfalme mpya wa wafalme na Bibi arusi wake. ( Ufunuo 19:11-21).

Muungano wa Miungano

Huu utakuwa muunganiko wa watoto wote wa Mungu, ambao sasa wamebadilishwa kuwa roho, wakifanana na Mungu na kumwona vile alivyo, anapojidhihirisha mwenyewe kwetu. Furaha ya kukutana na watakatifu wengine itakuwa ya msisimko. Nitabashiri hapa kidogo: ineonekana kwangu kwamba kwa namna fulani tutatambuana na kujuana. Nafikiri kwamba kimiujiza tutajuana na“kutambua” nani ndiye wa nani; angalau kati ya wale waliotangulia. Nasema hivi kwa sababu katika maono ya Mlima wa kubadilika sura Mlimani, Petro aliweza kuwatambua Musa na Eliya kwa namna fulani katika njozi wakiongea na Masihi ( Mathayo 17:1-4).

Hakuna ukumbi mzuri wa arusi kama Yerusalemu ya mbinguni, ambayo itakuwa jiji lako. Kwa taswira nzuri sana ya ajabu yake, sikiliza mahubiri ya Jeff Niccum “Taswira Kubwa” kwenye tovuti hii.

Tulipopanga mkutano wetu wa kwanza kabisa wa chuo kikuu, tabasamu na vicheko na furaha kuu ilikuwa ya kupindukia. Hiyo haitasimamisha mshumaa kwa kile ambacho tunakinena hapa! Hata haiwezi kuanzisha! Hatuwezi kufikiria Jiji lenye na urefu wa maili 1500 na upana wa maili 1500! Milima yetu yenye urefu sana ni maili 7 au 7.5 kwenda juu. Je, tutaweza kufikiria mji – mji war oho ambapo mitaa ya roho ni dhahabu ya kiroho, pamoja na malango ya lulu imara , pamoja na malaika wenye nguvu wanaokuja na kuondoka. Je, twaweza fikiria hiyo? Huo ni mji wako! Usikatishe tamaa kwa bakuli lolote la supu ya dengu!

Kwa nini tunazungumza juu ya hili leo ni kwamba ninaamini hili linafanyika siku ya Pentekoste – siku ile ile ambayo Mungu alioa Israeli, msimu ule ule angalau wakati Boazi na Ruthu walipooana, na wakati pete ya uchumba (Kigiriki arrabon- dhamana; inayo karibiana na arrabona –pete ya uchumba) ya Roho Mtakatifu ilipeanwa kwa mchumba siku ya pentekoste.

Ufunuo 19:5-7

Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu.

6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.

7 Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Wakati yote yamekwisha, mstari wa 11 unasema mbingu zikafunuka tena…na tunashuka duniani pamoja na Mume wetu, ambaye tumefunga ndoa naye hivi punde. Hebu tusome.

Ufu. 19:11-14

11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.

12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. [ Hawa majeshi ni kina nani wanaoandamana naye? Yuda anasema ni malaika na watakatifu wake. Hao ni sisi: Bi arusi wake, kanisa, wakitoka mbinguni]

Licha ya hayo tuliyoyasema, kuna mengine Zaidi kuhusu siku hii ya kusisimua:

  • Kuinua mikate miwili isiyochachwa kwa Mungu
  • Kupeana Torati katika Agano la kale na kupeana Roho katika agano jipya.
  • Mapokea ya Kiyahudi husema kila mtu alimsikia Mungu akiongea kwa lugha yake mwenyewe (kumbuka kulikuwa na mchanganyiko wa umati na Israeli). Siku iyo hiyo, jambo hilo-hilo lilitokea katika Matendo 2:2 kuhusu utoaji wa Roho wa Mungu.
  • Hata hivyo, katika agano la kale watu wapatao 3,000 walikufa mara baada ya Torati kutolewa (kisa cha ndama wa dhahabu) na katika agano jipya, watu 3,000 walipewa maisha mapya katika ubatizo. Katika Mlima Sinai,

Lakini ZAIDI ya hayo yote, Kuna MENGI Zaidi ambayo yanasisimua kuhusu siku hii:

  • Naamini siku hii, Siku ya Pentekoste, MALIPO YA KWANZA, fedha au dhamana ya Roho Mtakatifu italipwa yote tunapobadilishwa kwa roho. Wasioharibika wasioweza kudanganya na kutenda dhambi. Wasioweza kufa au kugonjeka au kuzeeka. Kutokufa. Kile ambacho watu wametafuta kitakuwa chetu kama zawadi ya Mungu.
  • Siku hii, au ikielekea siku hii, nafundisha kwamba tutachukuliwa na malaika wenye nguvu na kupelekwa kuwa na Masihi- ambaye atatuchukuwa pamoja naye hadi Yerusalemu ya mbinguni. Uko karibu kuenda kwa mwendo wa maisha-au pengine uingie hapo kwa kufumba na kufumbua. Bora kuliko “TIKETI YA MTANDAO” ya Disneyland ya “zamani”.
  • Katika siku hii, pentekoste, zaidi na zaidi kati yetu tunaamini kuwa tutakuwa tunaoa Mwana wa Mungu.
  • Katika siku hii, tutakuwa Mbinguni-mji wetu. Sio kuishi, lakini kwa muda na kurudi duniani kutawala duniani. Lakini nyumbani mwetu na Abba itakuwa Mbinguni daima. Alafu wakati utafika ambapo kutakuwa na mbingu mpya na nchi mpya-ulimwengu wa roho, dunia ambayo haitafanana sana kwa kipimo cha sayari hii ya kawaida inayooza. Na kwa wakati huo, kutakuwa na mbingu hasa hapa duniani, wakati ambapo Yerusalemu ya mbinguni inashuka toka kwa Baba hadi nchi mpya na HUU ndio utakuwa mji wetu katika nchi mpya.

Mungu iharakishe siku hiyo. Furahia kuhusu sikukuu-kwa sababu zote zahusu Mfalme na anachofanya kuwapa ufalme kwa watakatifu wake na jinsi atakavyoleta amani ya kudumu na furaha kwa ulimwengu wote. Mpaka wakati mwingine, huyu ni ndugu yenu katika Kristo, Philip Shields.