Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu - God’s holydays reveal his plan of salvation, Part 1

SEHEMU YA 1, Sikukuu za Mungu huonyesha mpango wake wa wokovu Pasaka kupitia Baragumu 

Maandiko yote ni NKJV isipokuwa kama yamebainishwa vinginevyo. 

MANENO MUHIMU: Baragumu, Yom Teruah, Rosh Hashanah, Pentekoste, Ufufuo wa kwanza, Mlima wa Mizeituni, harusi ya Mwana-kondoo, malimbuko, baragumu, kelele, mikate miwili, mpango wa wokovu

Maandiko yote ni NKJV isipokuwa kama yamebainishwa vinginevyo. 

MANENO MUHIMU: Baragumu, Yom Teruah, Rosh Hashanah, Pentekoste, Ufufuo wa kwanza, Mlima wa Mizeituni, harusi ya Mwana-kondoo, malimbuko, baragumu, kelele, mikate miwili, mpango wa wokovu

*********** 

Muhtasari: Sikukuu za Mungu ni kama ufunguo unaofungua mpango Wake wa wokovu kwa wanadamu. Huu ujumbe unatoa muhtasari wa kila sherehe kwa njia ya Baragumu, na msisitizo juu ya Pentekoste na Baragumu. Je, ufufuo wa uzima wa milele utatokea lini- siku ya Pentekoste au Baragumu? Kwa hiyo hutokea kwenye Sikukuu ya Milipuko (mara nyingi hutafsiriwa ―Tarumbeta‖)? Kusikiliza ujumbe huu kutasaidia kukutayarisha na kuwa tayari kwa Sikukuu za majira ya kuchepua ambazo ziko hapa na kufurahishwa na kile kilicho mbele yetu. Baragumu/Yom Teruah. Mahubiri zaidi yatakuja katika siku takatifu zilizosalia. 

**************** 

Mpango wa Mungu wa wokovu kwa wanadamu wote ni upi? Imewekwa mbele ya macho yetu kutoka sura ya kwanza ya Mwanzo hadi sura ya mwisho ya Ufunuo. 

Katika Mwanzo 1, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke kwa kipekee na kwa mfano wake na daada ya mfano wake (Mwanzo 1:26-28) na kuwapa wote enzi/ utawala juu ya nchi, pamoja. Mwanadamu ndiye kiumbe pekee cha uhai kilichoumbwa kwa mfano wa Mungu. Sisi ndio pekee ambao Mungu alitupulizia pumzi ya uhai. Vuimbe wengine wote hai kiurahisi waliumbwa kutoka kwa neno la Bwana (Zaburi 33:6-9, 148:5). 

Lakini Adamu na Hawa walipovunja amri ya Mungu na hawakuchagua Mti wa Uzima, kimsingi walimkabidhi ibilisi shetani funguo za ulimwengu kwa muda kuutawala- ingawa bado yuko chini ya mipaka ya mwisho iliyowekwa na Yehova. Biblia inamwita shetani ―mungu wa ulimwengu huu‖ (2 Kor 4:4). Hata Yeshua alimwita ―mtawala wa ulimwengu huu‖ (Yohana 14:30; 12:31). 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 2 

Lakini wakati wa parapanda ya 7, parapanda ya mwisho, watakatifu wateule wa Mungu watafufuliwa katika mwili wa kutokufa na kubadilishwa kuwa roho, tunasoma: 

Ufunuo 11:15 

Kisha malaika wa saba akapiga baragumu: pakawa na sauti kuu katika mbingu,zikisema,ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufamle wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele!‖ 

Hiyo tarumbeta ya saba 7, itasikika lini na yote haya kutokea na katika mlolongo upi? 

Hivyo karibu katika Light on the Rock. Mimi ni Philip Shields, mwenyeji na mwanzilishi wa tovuti hii ya bure. Ninaongeza nyenzo mpya kwa sehemu zote za VIDEO za mahubiri pamoja na toleo la sauti ya mahubiri, kwa hivyo kumbuka kusogeza chini na kutazama mahubiri na blogu juu ya mamia ya mada. Tuna mamia ya mahuburi hapa sasa pia. 

Kwa hivyo, turejee Mwanzo. Mwanamume na mwanmke walimsikiliza Nyoka akimhoji Mungu na kuwashawishi watende dhambi. Walikuwa wamechagua kumsikiliza shetani badala ya Mungu. Mungu alianza kutoa vidokezo vya mpango wa wokovu wa mwanadamu- lakini hakutoa tarehe wala ratiba. Shetani hajui yote. Yeye hajui kila kitu. Hapa ni kile ambacho Mungu alimwambia Nyoka-ambaye alikuwa shetani (Ufunuo 12:9)

Mwanzo 3:15 

―Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake, huo atakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino‖. 

Hapa tunaona unabii kuhusu kusulubishwa (kumponda kisigino) - lakini uzao wa mwanamke (Yeshua) ungemponda KICHWA shetani (Mwanzo 3:15).Wazee wetu walimkataa Mungu na hivyo wakafukuzwa kutoka bustani ya Edeni – maana yake‖ Bustani ya kupendeza, ya furaha‖ 

Wanadamu WOTE, waliokuwa ndani ya Adamu na Hawa- pia walitupwa nje na kwa mtu mmoja mauti iliingia ulimwenguni kwa njia ya dhambi kwa wanadamu wote(Warumi 5:12) 

Warumi 5:12 NIV 

―Kwa hivyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi‖ 

Lakini sasa kupitia Uzao wa mwanamke- Kristo, ubinadamu unaweza kurejeshwa kwa Mungu. Tutalichunguza hili kwa wakati mwingine- lakini kumbuka Kristo hakuzaliwa katika ukoo wa Adamu - lakini alizaliwa na Mungu Mwenyezi kupitia Roho Mtakatifu (Luka 1:32) Tutachunguza madokezo mengine yenye nguvu wakati mwingine. 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 3 

Mungu hakusema wakati Uzao wa mwanamke ungekuja. Kwa hiyo shetani alikuwa daima akitafuta Mbegu hii ili kumwua. Shetani hajui yote. Alidhania ile mbegu anaweza kuwa Habili, baada ya Mungu kuitakabali sadaka YAKE lakini si ya Kaini – ndivyo alivyofanya Kaini akamwua Habili ndugu yake. Kaini ―alikuwa wa yule mwovu‖ - 1 Yohana 3:12. 

Alijaribu kuua watu mbalimbali katika historia ambao huenda wakawa Uzao ambao ungeuponda kichwa cha shetani – kama Daudi, kama jamii nzima ya Wayahudi wakati wa Esta – yote katika jitihada za kuondoa Uzao (Kristo). Yeye bila mafanikio alijaribu kumwua Yeshua mara tu baada ya kuzaliwa, lakini Yeshua aliishi- ambaye alijitoa yeye mwenyewe kuwa fidia kwa ajili yetu sote na alitufungulia mlango wa kupokea wingi wa kibali/neema na zawadi ya haki yake. 

Kipawa cha haki yake hakizungumzwi kiurahisi na wengi, hasa katika makanisa na vikundi vya washika Sabato siku ya 7. Na kipawa si kitu unachoweza kukipata. 

Warumi 5:17 

―kwa maana kwa kukosa kwa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, (Adamu) zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema na kile kipawa cha haki watatawala kupitia uzima kwa yule Mmoja, Yesu Kristo‖. 

Lakini sisi inatupasa tuvitafute na kupokea hivi vipawa vya Mungu vya wingi wa rehema zake na VIPAWA vya haki yake (Soma Wafilipi 3:9-11). Ninayo mahubiri mengi ya jinsi - katika imani - haki ya Mungu inatolewa kwetu. Kwa hiyo sasa Mungu anawaita wachache kwa sasa - kuwa katika ufalme wake - na baadaye kila mtu ambaye yuko tayari kuitikia watafunguliwa akili zao kwa mara ya kwanza kabisa

Sikukuu za Mungu zinaelezea mchakato na wakati . Nitahakiki mchakato na mipango kupitia sikukuu hadi Sikukuu ya Baragumu. 

SIKU TAKATIFU ZA MUNGU na mavuno ya Israeli 

Mungu anatuambia wazi mpango wake ni nini - kupitia sikukuu zake 7, ambazo anaziita karamu ZAKE mwenyewe, moedim yake (Kiebrania) ikimaanisha miadi takatifu za Mungu. (Law.23:1-2). Hizi ni "sikukuu za Yehova" (mst.2), sio sikukuu za Wayahudi. Kanisa la awali la agano jipya kwa kweli lilianza kwenye mojawapo ya siku hizi takatifu -- siku ya Pentekoste (Matendo 2:1). Kanisa la kwanza lilishika wazi Pasaka na siku za Mikate isiyotiwa Chachu (1Kor. 5:7; 1 Kor. 11) – na Korintho, kumbuka kwa kiasi kikubwa lilikuwa kutaniko la watu wa mataifa. 

Miadi 3 ya kwanza ya Mwenyezi Mungu huanguka katika majira ya kuchipua/mapema majira ya kiangazi, na wanazingatia mavuno ya mapema au "malimbuko ya kwanza" kwa mwaka huo – kuanzia na Kristo kama malimbuko ya kwanza (1 Kor. 15:23) ikitangulizwa na Pasaka baadaye sadaka ya kutikiswa kwa maganda. Unaweza kutafuta mahubiri juu ya mada hizi kwenye tovuti hii - andika tu 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 4 

maneno 2-3 muhimu kama "Pasaka" au "Mganda wa kutikiswa" au ―Mkate Usiotiwa Chachu‖ au ―ninapoiona damu‖. 

Baada ya dhabihu ya Pasaka ya Yeshua kwa ajili yetu, basi siku takatifu huzingatia wale ambao Mungu anawaita sasa katika maisha haya -inayoonyeshwa na mavuno ya shayiri (na siku ya Mikate isiyotiwa Chachu) na kasha mavuno ya ngano ya Pentekoste au Shavuot, ambayo katika Israeli ni mwishoni mwa Mei au mapema Juni kwa kawaida. 

Na hatimaye, katika vuli ya mwaka, 4 za mwisho katika kalenda ya Kiebrania huangukia mwezi wa 7 wa Tishrei au Tishri. Hizi 4 za mwisho zinazingatia mpango wa Mungu kujidhihirisha na kuwaita kwake mwenyewe wanadamu wengine wote. 

JAMBO MUHIMU: Wengi huhifadhi sikukuu za moedim lakini wanaonekana kukosa kuonyesha ukweli kwamba sikukuu zinaelezea kwamba Mungu huwaita watu na vikundi - ―katika mpangilio wao wenyewe‖ kama Paulo anavyosema katika 1 Kor. 15:20-25. Unapaswa kusoma hilo. 

Nitaenda kwa kina juu ya hili katika siku zijazo, lakini pata hii: Ikiwa Mungu LAZIMA afikie kila mtu leo na kuwaleta kwenye wokovu kupitia Yeshua katika maisha haya - nani anashinda? Mungu au Shetani? 

Je, kweli unafikiri Mungu angeshindwa vita vyovyote na Shetani? 

Lakini kulingana na ni nani aliye na watu zaidi "kwa upande wake" - ni ushindi wa kukimbia kwa Shetani, hadi sasa, sivyo? 

Matendo 4:12 

―Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana HAKUNA jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu ambalo inatupasa kuokolewa kwalo." 

Lakini Mungu ana mpango wa kuokoa karibu kila mtu, isipokuwa wale ambao hawatamkubali Yeshua mara tu akili zao zitakapofunguliwa kwa mara ya kwanza. Wengi hajawai hata kusilikia jina "Yesu" au "Yeshua" kabla ya milenia. Wengi hawakuwahi kufunguliwa akili zao kuweza kuelewa, hata ikiwa walisikia kitu kuhusu Yesu Kristo. Tutazungumza zaidi kuhusu hili katika mahubiri mengine. 

Kuna ziwa halisi la moto, lakini linachoma watu, na wanakuwa majivu chini ya miguu ya wenye haki (Malaki 4:3). Mshahara wa dhambi ni MAUTI, si uzima wa milele kuchomwa kwa sehemu katika jehanamu ya moto na kuteswa milele na milele. 

Mungu atawaita watu kwenye wokovu kwa wakati wao, kwa mpangilio wao kama 1 Kor. 15:20- 25 inavyoeleza. 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 5 

Wale wanaoitwa SASA wanaitwa “malimbuko” ya wokovu (Yakobo 1:18). Wanaonyeshwa na sikukuu za msimu wa masika, ambayo yote ni kuhusu “malimbuko” kulingana na maandiko mengi. 

Sikukuu ya kwanza ya Vuli ni Sikukuu ya Baragumu - Yom Teruah kwa Kiebrania, ikimaanisha Siku ya Milipuko/baragumu/vigelegele. Ninaamini katika ibada zetu za kanisa leo tunapaswa kupiga kelele za sifa zake na kupiga shofa siku hii. 

Wayahudi kwa makosa huita Sikukuu ya Baragumu/milipuko -- Rosh Hashanah, ikimaanisha "kichwa cha Mwaka", jina ambalo halijatumiwa katika Maandiko kwa sikukuu hii na SIYO Mwaka mpya. Mwaka mpya wa Mungu huanza katika msimu wa kuchipua (Kutoka 12:1-2). MUNGU MWENYEWE alisema kwamba mwezi wa Abibu ulikuwa mwezi wa kwanza wa mwaka kuanzia wakati huo na kuendelea. 

Kutoka 12:1-2 

Basi YHVH akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, na kuwaambia, 2 ―Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa mwezi wa kwanza wa mwaka kwanu.” 

Mungu anaita Sikukuu ya Milio/Sikukuu ya Baragumu, siku ya kwanza ya mwezi wa SABA, sio mwezi wa kwanza! Hivyo mapokeo ya Kiyahudi kwamba mwaka wao mpya ni Rosh Hashanah (―kichwa cha mwaka‖), haitegemei Biblia bali mila zao wenyewe. Kumbuka Yeshua alihubiri dhidi ya mapokeo yao ambayo yalichukua watu mbali na sheria ya Mungu! (Mathayo 15:3-6). 

Mambo ya Walawi 23:23-24 

―Ndipo YHVH akanena na Musa, na kumwambia, 24 Nena ―na wana wa Israeli, waambie: ‗Mwezi wa SABA, siku ya kwanza ya mwezi huo, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu.‖ 

Tarehe za 2023 za Baragumu/Upatanisho 

Hizi ndizo tarehe za 2023, kulingana na kalenda unayochagua – Kalenda ya Jadi ya Rabi au wale wanaoenda kwa kuona mwezi mpya huko Yerusalemu. Na Wayahudi wa Orthodox wataadhimisha sikukuu hii kwa siku 2. Tunafanya kile Mungu anachosema na kuadhimisha kila moja kwa siku ambayo tumeambiwa tushike kila moja. 

MNAMO 2023 - na tarehe hubadilika kwenye kalenda yetu ya Gregorian kila mwaka – hizi ni tarehe za siku takatifu za Vuli: Kumbuka Sabato za Mungu hutunzwa kutoka machweo ya jua ―siku iliyotangulia‖ hadi machweo ya sikukuu. KWA HIYO Sabato ya kila wiki hudumishwa kila mara machweo ya Ijumaa usiku hadi machweo ya Jumamosi usiku, kwa mfano. 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 6 

Sikukuu ya Baragumu/Yom Teruah/Rosh Hashana - Kalenda ya Marabi Septemba 16, 2023.Wayahudi wa Orthodox Kwa hakika wanaitunza kwa 2 siku (Sept 16 na Septemba 17, kuanzia machweo Septemba 15 hadi machweo Sept 17.) Ingawa kwa wengi wetu, tunaitunzasiku moja kama Mungu alivyosema, kuanzia Ijumaa usiku tarehe 15 Septemba machweo ya jua hadi Jumamosi usiku Septemba 16, 2023. 

Itakua tofauti katika mwaka wa 2024 na zaidi. 

Kuna wale wanaoenda kwa kuonekana kwa mwezi mpya huko Yerusalemu. Mara nyingi hakuna tarehe hususainayoweza kuwekwa ikiwa hakuna mtu anayeona mwezi mpevu wa kwanza inapotarajiwa huko Yerusalemu. Inaweza kuwa na mawingu sana, giza au mvua. Kwa hivyo tarehe inaweza kuhamishwa. 

Lakini SISI tutaadhimisha Baragumu mnamo Septemba tarehe 16, 2023 Siku ya Jumamosi. 

Ikiwa ungependa kwenda kwa mwonekano wa kwanza wa mwanga wa mwezi mpya huko Yerusalemu, basi kuna uwezekano kwamba Baragumu itaadhimishwa mnamo mwaka wa 2023 mnamo tarehe 17 Septemba. 

Kumbuka kwamba ―mwezi mpya‖ katika maneno ya Biblia si giza la mwezi, kama tunavyofanya katika jamii za kimagharibi, lakini ni mwanga wa kwanza unaoonekana au utepe wa mwezi. Kumbuka kwamba Mungu alitupa mwezi na jua kwa ajili ya NURU na kwa ajili ya kuamua ―moedim‖- siku Takatifu za Mungu. 

Mwanzo 1:14 NKJV 

―Kisha Mungu akasema, iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana; nayo iwe kwa ajili ya dalili na majira, na siku na miaka;‖ 

Mwanzo 1:14 

Kisha Mungu akasema, ―Na iwe mianga katika anga ili itenganishe mchana na usiku. Itakuwa ishara kwa sikukuu na siku na miaka.‖ 

Mnamo 2023, hizi zitakuwa tarehe za kitamaduni za sikukuu zilizosalia. 

Siku ya Upatanisho, Yom Kippur, siku ya mapumziko kamili na kufunga kuanzia machweo ya Septemba tarehe 24 hadi machweo ya tarehe 25 Septemba. Siku ya upatanisho, Yom Kippur, ni tarehe 25 Septemba. Wayahudi huadhimisha siku hii takatifu kwa siku moja tu. Tunafanya vivyo hivyo. 

Wale wanaoenda kwa kuonekana kwa mwezi mpya huko Yerusalemu huenda watakuwa wanaadhimisha Upatanisho mnamo 2023 mnamo Jumanne, tarehe 26 Septemba. Ninasema ―huenda‖ kwa sababu yote yatategemea ikiwa mtu anauona mwanga wa mwezi au la. Ikiwa ni giza, mawingu, au mvua, hawataiona. 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 7 

Tutakuwa tukiadhimisha Upatanisho tarehe 25 Septemba Jumatatu kuanzia machweo ya Jumapili usiku wa tarehe 24 Septemba hadi machweo ya tarehe 25 Septemba. 

Ni siku ya mapumziko kamili na kufunga. Hatuli au kunywa kwa masaa 24. Tazama Sehemu yangu ya 2 kwenye sikukuu za Vuli. Pia unaweza kupata mahubiri kuhusu siku ya Upatanisho kwa kutumia tu Upau wa Kutafuta kwenye tovuti yangu na uandike ―Siku ya Upatanisho‖ 

Sikukuu ya Vibanda itaanza tarehe 30 Septemba 2023, Jumamosi. Sikukuu ya mwisho ya 2023 ni “siku ya 8” tarehe 7 Oktoba, Jumamosi, 2023. 

Pasaka -Siku ya Pasaka, 14 Nisan/Abibu - sio sikukuu bali ni sehemu muhimu ya mpango wa Wokovu. 

Nina mahubiri mengi juu ya Pasaka, kama vile "Ninapoona damu", kutolewa utumwani kutoka Misri - ikionyesha damu ya Kusulubiwa ya Yeshua anayetukomboa kutoka kwa utumwa wa shetani juu yetu. Tumia tu upau wa Utafutaji kwenye ukurasa wa nyumbani na uandike maneno 1-3 tu. Alitukomboa kutoka dhambi zetu zote na kututoa mikononi mwa utumwa kiroho. Kwa kumkubali, tunakubali kwa imani haki ya Mungu mwenyewe iliyohesabiwa kwetu na tunakuwa WAKE. 

SIKU ya Pasaka sio siku kuu, lakini jioni hiyo mwishoni mwa siku ya Pasaka NI siku ya kwanza ya Mikate isiyotiwa Chachu na ni sikukuu. 

LAZIMA tuelewe kwamba katika Pasaka ya mwisho ya Yeshua - ndivyo alivyoiita – alisema, ―Fanyeni hivi kwa ukumbusho WANGU‖ (Luka 22:19; 1 Kor. 11:24-25). Mwana-Kondoo, akiokolewa kutoka utumwani, akitoka Misri -- YOTE HAYO yalielekeza KWAKE. 

TUNAPO chukua Pasaka, LAZIMA tuelekeze kwa Kristo! Lakini wengi hutumia muda mwingi Misri, pigo la 10, nk, badala ya kufanya kile Kristo alisema. Zungumza juu ya YAKE, Mwana-Kondoo wa Mungu, sio sana kuhusu wana-kondoo katika Misri. WANA-KONDOO walimwashiria Yeshua. Hakuna mahali popote ambapo kuna rekodi ya Yeshua katika PASAKA YAKE ya mwisho inazungumza kuhusu Farao na Misri na hayo yote—kwa sababu hiyo ilimhusu YEYE sasa. 

Siku za Mikate Isiyotiwa Chachu – siku ya kwanza na ya mwisho ni sikukuu - wakati tumekombolewa na Kristo, maisha yetu yanahitaji kutoka katika maisha ya dhambi imeashiriwa na mkate uliotiwa chachu. Tunakula mikate isiyotiwa chachu kila siku, ikionyesha kumchukua Yesu Kristo kama chakula chetu, riziki yetu. Mkate usiotiwa chachu hauonyeshi kuwa wewe au mimi ni wenye haki - lakini Yeshua ndiye mwenye haki kabisa - ambaye tunampokea kila siku. Ingawa bado sisi tunajikwaa katika dhambi, sio njia ya 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 8 

maisha yetu tena. Yeshua ni maisha yetu sasa. Yeye ni mkate wa haki usiotiwa chachu. 

Huo ni utofauti ambao haufanyiki kila wakati. Mkate usiotiwa chachu unamhusu Yeshua. Yote ni kuhusu Yeshua kufanya njia iwezekane kwa ajili yetu. Haituhusu. 

SADAKA YA SIKUKUU 

Kumbuka tunapaswa kutoa matoleo ya sikukuu mara 3 kwa mwaka - Sikukuu ya Mikate isiyotiwa Chachu, Pentekoste, na Sikukuu ya Vibanda. (Kumbukumbu la Torati 16:16-17). Saidia ushirika ambapo unalishwa. Ndiyo, tunakubali matoleo ya sikukuu kusaidia kulipia kazi tunazofanya. Huduma nyingi za utunzaji wa siku takatifu huchukua sadaka katika kila Sikukuu. Maandiko yanasema mara 3 kwa mwaka, kwa hivyo mimi binafsi SIFUNDISHi matoleo ya sikukuu kwa kila sikukuu 7, mara 3 pekee kwa mwaka - kama vile Biblia inavyosema. 

Kumbukumbu la Torati 16:16-17 

"Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote watahudhuria mbele za BWANA Mungu wako mahali atakapochagua: katika Sikukuu ya Mkate usiotiwa Chachu, katika Sikukuu ya Majuma, na katika Sikukuu ya Vibanda; wala wasionekane mbele za YHVH mikono mitupu

17 Kila mtu atatoa kadiri awezavyo, kulingana na baraka ya YHVH Mungu wako ambaye amekupa.‖ 

Tarehe inatofautiana, lakini kuna Siku ya Miganda ya Kutikiswa, inayoonyesha Kristo, kama shayiri ya malimbuko ya kwanza ambayo ilipaswa kukubaliwa na Mungu. Lakini pia ilimwakilisha Kristo akituwasilisha sisi, kama malimbuko yaliyosalia, kwa Baba aliye mbinguni, ili tupate kukubaliwa kwa niaba yake (Law 23:9-11). 

Kwa sababu ya Masihi - hata wewe na mimi, bila kujali jinsi gani tumekuwa wabaya, tunapomkubali Yeshua, tunakubaliwa na Baba - kwa niaba ya Kristo. Siku ya Mganda wa Kutikiswa sio sikukuu lakini kazi rasmi huanza ya kuvunwa kwa shayiri iliyosalia, mkate wa mtu mnyenyekevu. 

PENTEKOSTE/SHAVUOT/SIKUKUU YA WIKI, SIKU YA MALIMBUKO 

Kisha tuna hesabu ya siku 50 hadi Pentekoste/Shavuot na mavuno ya ngano ya mapema, ikionyesha wale wote ambao Mungu anafanya nao kazi sasa na kuwaita kwenye wokovu sasa. Pentekoste pia inaitwa Sikukuu ya Majuma, Siku ya Malimbuko ya kwanza, Shavuot (ikimaanisha "wiki") na Pentekoste - inamaanisha "50" (sio "hesabu 50"). 

Kutoka 34:22 

―Nanyi mtaitunza sikukuu ya majuma, nayo ni MALIMBUKO ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Kukusanya mwisho mwa mwaka.‖ 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 9 

Hesabu 28:26 

―Tena katika siku ya MALIMBUKO, hapo mtakapomsogezea Bwana sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi‖ 

Mikate 2 ya kutikiswa iliyoinuliwa kwenye Pentekoste ilionyesha nini, tena? 

Mambo ya Walawi 23:17 

―Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe MALIMBUKO kwa YEHOVA‖. 

TAZAMA jinsi malimbuko yanavyohusika sana hadi Pentekoste. Neno halitumiki kwa njia yoyote kwa Baragumu au kwingineko. Ufufuo wa kwanza kumbuka, ni kuhusu ufufuo wa malimbuko ya kwanza ya WATEULE wa Mungu. Limbuko la Waliochaguliwa wanaelekeza kwenye Pentekoste. Tunaendana na maana ya malimbuko ya kuchipua ya sikukuu. 

Kwa hivyo ninaona Pentekoste kama sikukuu ya MAPINDUZI, namaanisha kwamba ninaamini kuwa yametimizwa tayari, lakini bado haijakamilika kabisa. 

Hapa kuna kile ambacho tayari kimetokea: 

• Pentekoste ilikuwa wakati Yehova alipowapa Israeli Torati (sheria, maagizo) katika Mlima Sinai (Kut 20-24) 

• Katika Agano Jipya, Mungu alimimina Roho wake Mtakatifu - muhuri wake wa ahadi ya kukamilisha kile kilichoanzishwa ndani yetu (Matendo 2) 

Mungu alioa Israeli kwenye Mlima Sinai siku ya Pentekoste (Kutoka 24:3-11), kwa hivyo muundo wa wakati harusi inafanyika umewekwa. 

• Kuna uwezekano mkubwa Ruthu na Boazi walifunga ndoa mnamo au karibu na Pentekoste, mwisho wa mavuno ya shayiri na ngano (Ruthu 2:23) 

Acha nirudie: Siku ya Pentekoste palikuwa na mikate miwili mikubwa iliyotiwa chachu (Law 23:15-17) iliyoinuliwa juu na Kuhani Mkuu na kisha kushushwa tena. Maandiko yanatuambia mikate inawakilisha nini: 

Mambo ya Walawi 23:17 

―Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa YHVH.” 

Kwa nini ninatumia muda mwingi kwa hili, kuonyesha Pentekoste inahusu malimbuko? Malimbuko kamwe hayafungwi na Sikukuu ya Baragumu/Yom 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 10 

Teruah.Kamwe. Lakini WANAFUNGWA na Pentekoste. Na malimbuko ni akina nani? Ni SISI – 

Yakobo 1:18 

―Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.” 

Kwa hivyo Pentekoste/Shavuot ni wazi kuhusu kuonyesha watu walioitwa MALIMBUKO YA KWANZA. Hii ni muhimu kuelewa ili tupate Pentekoste na Sikukuu ya Baragumu sahihi na wakati wa Ufufuo wa Kwanza kutokea. 

Paulo alitaja mara nyingi Wakristo wa mapema kuwa ―malimbuko ya kwanza‖ (Warumi 16:5; 1 Kor. 16:15; Warumi 8:23). Yohana anazungumza juu ya wale 144,000 baada ya ufufuo wao - kuwa mbinguni kama malimbuko (Ufunuo 14:4). 

Matukio lazima yaambatanishwe ipasavyo na siku yake maalum katika siku ya Kalenda ya Mungu. Sikukuu za kuchipuka ni kuhusu malimbuko ya kwanza – na hao ni sisi. Sikukuu za vuli sio juu ya malimbuko. 

Kwa hiyo ufufuo wa kwanza unahusu ufufuo wa malimbuko

Kwa hivyo, wengi wetu tunaamini zaidi na zaidi kwamba tarumbeta ya 7 italia, na ufufuo wa kwanza utatokea siku ya PENTEKOSTE; si kwenye Baragumu

Pentekoste pia ilikuwa wakati Mungu alioa Israeli. Kwa hivyo atamwoa bibi harusi wake - kanisa (Efe5:25-33; 2 Kor. 11:2) kuna uwezekano mkubwa pia siku ya Pentekoste, ikajumuishwa na karamu ya Arusi ya Mwana-Kondoo juu mbinguni; haya yote kwenye Pentekoste, si Sikukuu ya Baragumu. 

Kumbuka shofa, tarumbeta zilipulizwa kwenye sikukuu zote ili ukweli uwe kwamba Sikukuu moja inayoitwa "Sikukuu ya Baragumu" haiwezi kushawishi yenyewe kwamba tarumbeta ya 7 hutokea siku hiyo. Na hata hivyo, maana halisi ya Yom Terua ni kelele, kelele za shangwe, na sauti kuu. 

Nina mahubiri kwenye tovuti hii kuhusu Harusi ya Mwana-Kondoo, siku ya Pentekoste, na ―naenda kuwaandalia mahali‖. 

Tena, kwa nini nadhani ufufuo na ndoa kwa Kristo inafanyika siku ya Pentekoste? (Na kwa nini naita hii ni sikukuu ya mpito – imetimizwa kwa sehemu tu hadi sasa, kama ninavyoona). 

• Bado kuna mapigo 7 ya mwisho ya bakuli ya kutekelezwa baada ya tarumbeta ya saba kupigwa. Haya mapigo 7 ya mwisho ya bakuli (Ufunuo 16) yatachukua muda, pengine angalau miezi 3 au 4, ikiwa ni pamoja na milioni 200 kuja kutoka mashariki kuvuka Frati ili kupigana na Kristo. Ikiwa ufufuo ungekuwa umetokea kwenye Baragumu, Kristo na Kanisa watakuwa wanafanya nini wakati wa Mapigo 7 ya mwisho ya bakuli yanatokea? 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu inaendelea 11 

Nasema anamchukua bibi arusi wake mbinguni kuolewa, kama Isaka (mfano wa Kristo) alimchukua Rebeka ndani ya hema ya mama yake na kukamilisha ndoa yao. Tazama Wagalatia 4:21-26 inalinganisha hema la Sara na mbinguni. 

Yesu, Mwana mzaliwa wa kwanza wa Mungu kati ya ndugu WENGI, hana budi kuoa Bibi-arusi ambaye ni wa aina sawa na yeye. Ataoa wengine ambao pia ni watoto wa kweli wa Mungu, kama mwili MMOJA, kama vile Kristo alivyo Mwana wa Mungu. 

• Siku za kuchepua na Pentekoste huonyesha limbuko la kwanza kwa Mungu. Sisi ni malimbuko. Sikukuu za Vuli, hata hivyo, zinahusu kuleta mavuno makubwa, ikionyesha wale ambao wataitwa baadaye. Wao si malimbuko. Sikukuu zinapaswa kuendana na kiashirio. Wale watakao mwoa Yeshua watakuwa malimbuko. 

SIKUKUU YA BARUGUMU/YOM TERUAH 

Kwa hivyo hebu tuende sasa kwa Yom Teruah, INAYOITWA kwa kawaida Rosh Hashana (Kichwa cha Mwaka), lakini kitenzi chake katika Biblia ni Yom Teruah. ―Yom‖ = SIKU, na ―Teruah‖ maana yake ni siku ya ―KELELE, milipuko za SHOFA, mlio wa tarumbeta, hulia kwa sauti kubwa.‖ 

Kwa maoni yangu, kwa hadithi fupi ni kwamba siku hii inawakilisha kurudi kwa Yeshua pamoja na watakatifu wake ambao tayari wamefufuka, ambao kwa sasa pia tayari amewaoa mbinguni. Sasa wanarudi DUNIANI pamoja, kupigana na majeshi waliokusanyika na kutua kwenye Mlima wa Mizeituni na kuchukua hatamu za serikali ya dunia. 

Nina mahubiri kadhaa yaliyochapishwa ambayo yanasimulia kile kinachopaswa kutokea kabla Kristo kurudi kwenye Mlima wa Mizeituni, kwa hiyo sitarudia hayo yote tena. 

Sasa maelezo zaidi. 

Hadithi za Kiyahudi kuhusu Yom Teruah/Tarumbeta/Rosh Hashanah 

INAWEZEKANA kwamba uumbaji ulianza katika kile ambacho tungekiita wakati huu wa mwaka, kisha ilibadilishwa na Mungu katika Kut. 12:1-2 kuwa katika majira ya kuchipua. Mila ya Kiyahudi ni kwamba ilikuwa siku 1 ya mwezi wa 7 wa Mungu (kawaida Septemba) ndipo Mungu alipoumba Adamu na Hawa. Wayahudi huiweka kama siku 2, mnamo 2021 kutoka Jumatatu usiku Septemba 6 kupitia Jumatano usiku Septemba 8, ili kuwa na uhakika kuwa wana siku sahihi. Wayahudi wanapiga shofa kila asubuhi ya siku hizo 2, kula milo ya sherehe, na kuwasha mishumaa kila jioni. Wanapenda tufaha zilizowekwa kwenye asali usiku wa kwanza, kisha kitu kingine usiku wa 2. Kuna maazimio mapya ya mwaka na kwa ujumla wakati wa sherehe. Kuna milipuko mingi ya shofa, kwa jumla ya karibu 100. Sheria nyingi, mapokeo mengi ya kitamaduni - lakini tunafuata yale ambayo maandiko yanasema. 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 12 

Amini usiamini, kati ya sikukuu 7, sikukuu ya Baragumu/Yom Teruah imesemwa MACHACHE zaidi kuihusu, kuliko sikukuu nyingine yoyote. 

Kwa hivyo, TURUDI NYUMA kidogo na tupate mwendelezo hadi leo: 

Ninaamini, kwa ufupi, kwamba tunabadilishwa kuwa roho au kufufuliwa katika roho kwa tarumbeta ya 7 ya mwisho (Ufu. 11:15), ambayo naamini inatokea kwenye Sikukuu ya Pentekoste, si Sikukuu ya Baragumu, kukutana na Kristo katika mawingu ya mbingu yetu ya kidunia - na kisha tunachukuliwa hadi Yerusalemu ya Mbinguni mara moja kukutana na wengine katika ufufuo wa kwanza kuanzia Habili na kuendelea- na kuwa na karamu ya Harusi ya Mwanakondoo. 

(Ninarudia - kwa sababu tumekuwa tukisisitiziwa sana kuwa ufufuo hutokea kwenye Baragumu, nadhani mara nyingi ni kwa sababu inaitwa Sikukuu ya ―TARUMBETA‖. Kwa hiyo nataka kuwa na uhakika kwamba sote tunapata matatizo na mafundisho hayo. Haina maana) 

Ninaamini watakatifu waliokwisha kufufuka kisha wanarudi pamoja na Kristo kutoka kwa karamu yao ya arusi ya mbinguni (Ufu 19) KATIKA siku hii, Siku ya Milipuko – kwa kuondoa majeshi ya chini na kuchukua serikali. 

Na ikiwa haya yote yatatokea katika Yom Teruah, ingawa sauti za tarumbeta za MUNGU zitakuwa zimekamilika kwa muda, kutakuwa na shofa mingi na mingi na mingi itakayopulizwa katika Israeli na duniani kote siku hii! ITAKUWA kweli Sikukuu ya Milipuko na vifijo! Kwa sababu ndivyo Wayahudi na wengi wetu tunavyoshika sikukuu za Mungu HUFANYA! Tutapiga kelele kwa furaha tutakapopiga shofa zetu! Mara mingi katika siku hii. 

Tena, kumbuka, shofa, tarumbeta za fedha zilipulizwa kwenye sikukuu ZOTE (Hesabu 10:10). 

Lakini kabla ya kurudi tena, tukiwa mbinguni, bakuli 7 ya mwisho ya mapigo ya Ufunuo 16 yanamiminwa. Pigo la bakuli la 6 linachukua muda mrefu – miezi - kuhamisha watu milioni 200 kutoka mashariki, kuvuka Mto Frati uliokauka huko Iraqi - hadi Israeli ili kupigana na Mungu anaporudi kama Neno la Mungu. 

Hebu tusome kuhusu bakuli # 6 na 7 katika Ufunuo 16, ambayo hutokea BAADA ya Baragumu ya 7, parapanda ya mwisho (Ufunuo 11:15). 

Ufunuo 16:12-21 

Na huyo malaika wa sita akamimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafamle watokao katika mawio ya jua. 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 13 

13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 

14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita vya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. 

15 ―Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake‖ 

16 Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har- Magedoni. [Bonde la Megido] 

Kitasa cha Saba: Dunia imetikisika kabisa 

17 Na huya wa saba akikimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu la mbinguni, katika kile kiti cha enzi, ikisema, “imekwisha kuwa”. 

18 Pakawa na umeme na ngurumo na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyo kubwa tetemeko hilo. 

19 Na mji ule mkuu ukagawanyika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 

20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta(Zaidi ya uzito wa pauni 100), ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno. 

Kwa hivyo kufikia wakati huo, tutakuwa tumefufuliwa kama Bibi-arusi wa kiroho kwa Kristo, tumeolewa na Yeshua, na sasa tunarudi chini - lakini wakati huu, sio katika mawingu lakini juu ya farasi wa roho (malaika) kupigana na majeshi yaliyokusanyika chini kama UFU. 19 inavyosema

Ninaamini KURUDI huku - wakati huu na Mfalme Yeshua AMEOLEWA na Bibi arusi wake, malimbuko ya Mungu -- kutatokea Siku ya Baragumu, tunapotua kwenye Mlima wa Mizeituni upande wa mashariki wa Yerusalemu. 

KUFIKIA wakati huu, anga itakuwa GIZA na kufunikwa na MOSHI na majivu kutoka kwa vita, milipuko ya volkeno, mioto - na kujaribu kuona mwanga wa kwanza kutoka kwa mwezi inaweza kuwa karibu na haiwezekani. MPIGO WA SUMAKU WA UMEME (EMP) unaweza kufuta elektroniki zetu zote. Hatuwezi hata KUONA jua au 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 14 

mwezi kwa wiki kadhaa - na inaweza kuwa ngumu sana hata kujua ni SIKU gani! Pigo la bakuli la 5 la UFU. 16 ni GIZA chungu kuweza kumbuka. 

Kwa hivyo tunarudi, naamini kwenye BARAGUMU/Yom Teruah - au Rosh Hashana ya Wayahudi: Mlima wa Mizeituni utapasuka katikati na bonde pana sana kuundwa. Miili ya wale milioni 200 itayeyushwa kwa jinsi Kristo anavyopigana nao. Zek 14:12-13 - isome. Zekaria 14 ni somo la lazima kwako. 

Kutakuwa na KELELE kubwa za FURAHA kwa upande wetu ili hatimaye kuuondoa ulimwengu huu kwa viongozi wanaotawaliwa na Shetani na mapepo yake, kama nilivyosoma… na kuanza utawala mpya wa Milenia wa Yesu Kristo na Bibi-arusi wake duniani. 

TENA – ikiwa UFUFUO wa kwanza ni kwenye sikukuu ya Baragumu, sisi sote tunafanya nini wakati Mapigo ya 7 ya mwisho ya bakuli yanamiminwa? Hiyo itachukua angalau miezi 3-au 3-1/2! Harusi ingefanyika wapi isipokuwa kwenye Bahari ya Kioo au hekalu la mbinguni? Na Mathayo 22:1-2 inasema MFALME (MUNGU) anaandaa harusi ya mwanawe. Mungu yuko wapi? MBINGUNI. Tunaomba ―Baba yetu aliye mbinguni”. 

Na sikukuu za majira ya Vuli huashiria wokovu wa wanadamu wengine wote. Pentekoste inaitwa "Siku ya malimbuko" -- (Hesabu 28:26). Mikate 2 iliyotiwa chachu kuinuliwa juu siku ya Pentekoste, pia huashiria malimbuko, Biblia inasema. (Mambo ya Walawi 23:17). Na SISI pamoja na roho ya Mungu ni malimbuko! Yak 1:18. Hivyo Pentekoste inalenga malimbuko - na hiyo labda ni wakati wa ufufuo kutokea. 

Mambo ya Walawi 23:23-24 

― Kisha YHVH akanena na Musa, na kumwambia, 24 nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi,kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu.” 

Kwa Kiebrania, “kupuliza” ni Teruah – milipuko, kelele, milio ya tarumbeta, n.k. Haya ndiyo "Kamusi Kamili ya Kusoma Neno ya Agano la Kale": 

Strong’s word 8643. Teruah -- Nomino ya kike inayoonyesha mlio wa furaha; kelele za kengele, kelele za vita. Inaashiria sauti kubwa, kelele kali au kulia kwa ujumla, lakini mara nyingi inaonyesha kelele ya furaha au ushindi (1 Samweli 4:5, 6); sauti kubwa inayotarajia tukio linalokuja (Yoshua 6:5, 20). Inaweza kurejelea kelele au ishara iliyotolewa na chombo (Mambo ya Walawi 23:24; 25:9). Amosi alitumia neno hilo kurejelea kelele za vita (Amosi 1:14; 2:2; taz. Ayubu 39:25; Sefania 1:16). Bwana huweka kelele za furaha ndani ya watu wake (Ayubu 8:21; 33:26). 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 15 

Ninaamini tunapaswa kupiga shofa siku hii katika ibada zetu za kanisa. 

KWANINI kelele? Kwa watoto wa Mungu, ni shangwe. Kwa ulimwengu ambao umekuwa ukimlaani Mungu kupitia mapigo yote (soma tu Ufunuo), ni kelele za hofu, laana, vilio vya kukata tamaa. Hatimaye bila shaka, baada ya muda - Yeshua na Bibi-arusi Wake watatengeneza, kurejesha na kujenga upya ulimwengu wa ajabu. Tutajadili hilo zaidi tunapozungumza wakati ujao kuhusu Sikukuu ya Vibanda. 

Mambo ya Walawi 23:24 CJB 

“…katika mwezi wa SABA [si wa kwanza]‖ Siku ya kwanza ya mwezi, itakuwa kwenu siku ya kustarehe kabisa ya ukumbusho, ni kusanyiko takatifu unaotangazwa kwa milipuko za shofa.‖ 

Wayahudi hutumia Rosh Hashana - Sikukuu ya Milipuko/tarumbeta - kama siku ya kwanza ya"siku 10 za Kicho", ambayo inaisha na Upatanisho na hukumu, kama wanavyoiona. Ninaweza kushughulikia dhana hii zaidi katika mahubiri yajayo. 

Kwa hiyo sikukuu za majira ya Vuli za Mungu zinaonyesha wakati ambapo Mungu anaitikisa dunia na watu wote ndani yake—na bila shaka tunataka kuwa sawa na Mungu, karibu na Mungu, kumtafuta Mungu, kuliko hapo awali. 

Ni siku ya milipuko, kupiga kelele kwa furaha na kuonyesha msisimko fulani kwa ajili ya Kristo hatimaye kuja kutawala, kwa kweli, labda kwa nyakati zetu za maisha. Nina umri wa miaka 68, kwa hivyo nina hakika nikitumai atarudi kabla sijafikisha miaka 80, lakini atakapokuja ni sawa kwangu. 

Ulimwengu - haswa Wayahudi - watafurahi sana KUONDOLEWA katika utumwa na kuteswa kwa nguvu ya Mnyama inayokuja ya ulimwengu - hiyo kwenye Yom Teruah mwaka atakaporudi Kristo, bila shaka kutakuwa na kelele nyingi za furaha, kusherehekea, na kupiga shofa zao wenyewe wanapomwona Masihi wao, yule Myahudi kutoka Nazareti akija na jeshi lake la malaika watakatifu na Bibi-arusi wake, kuwaokoa . Hii itakuwa SIKU ya uhakika wa MLIPUKO atakaporudi na kutua kwenye Mlima Mizeituni. 

Ingawa kwa ulimwengu wote, kurudi kwa Mwana wa Mungu - wakati huu na uweza na mamlaka, na kama Mfalme wa Wafalme, itakuwa siku atakapoonyesha ghadhabu na adhabu kwa wale wanaoiangamiza nchi. Nitashughulikia hilo zaidi mwaka ujao. 

Maandiko yanarejelea kipindi cha mwaka mmoja kabla ya Kristo kutua kwenye Mlima wa Mizeituni, kama "SIKU ya BWANA", na mara nyingi "siku ile" inarejelea wakati huu kipindi pia, kikiongoza hadi Mfalme wetu kutua kwenye Mlima wa Mizeituni. 

Sehemu ya 1, Muhtasari wa sikukuu za kwanza zinazoonyesha mpango wa Mungu wa wokovu, inaendelea 16 

Amosi 5:18 

“Ole wenu ninyi mnaotamani siku ya BWANA!…Itakuwa giza na wala si nuru.” 

Kwa hivyo kwa watu wengine, itakuwa wakati mbaya wa tauni, giza, matetemeko ya ardhi, vita, na mvua ya mawe - na kelele zao zitakuwa za hofu na za kutisha. Kwa wakati, watapata kwamba ni jambo zuri Yeshua amerejea. 

MAOMBI YA KUFUNGA.